Klabu ya Young Africans leo imemtangaza Shaban Katwila kuwa Meneja wa
Timu A na Baraka Kizuguto kuwa Afisa Mawasiliano wa klabu, kujaza
nafasi zilizkokuwa wazi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Katibu Mkuu wa
klabu ya Yanga Lawrence Mwalusako, amesema kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichoketi mwishoni mwa wiki kiliwapendekeza Katwila na Kizuguto
kushika nafasi hizo zilizokua wazi.
Katwila anakuwa Meneja wa timu
kufuatia kuwa wazi kwa nafasi hiyo baada ya aliyekuwa meneja wa timu
Hafidh Saleh kuhamishiwa idara ya Mipango na Usafirishaji na Kizuguto
anachukua nafasi iliyokua wazi kufuatia Louis Sendeu kumalizika kwa
mkataba wake.
Aidha Mwalusako alisema Katwila ana uzoefu na
masuala ya mpira, alikuwa mchezaji wa Yanga kwa kipindi kirefu, alikuwa
Nahodha wa timu ya Yanga na timu ya mkoa wa Dar es Salaam kwa vipindi
tofauti hivyo anauelewa na masuala ya mpira na atakua kiunganishi kizuri
kati ya Uongozi na wachezaji.
Kizuguto ana taaluma ya Teknlojia,
Habari na Mawasiliano hibyo Kamati ya Utendaji iliona anafaa kushika
nafasi ya Habari na Mawasilliano, kwa kuwa ana uzoefu na masuala ya
mawasiliano ya jamii kufuatia kazi hiyo kwa muda mrefu alisema
'Mwalusako'
Naye Katwila alishukuru kwa uongozi kumwamini na kumpa
nafasi hiyo, na kusema anaamini ataifanya vizuri ipasavyo kwa kuwa ana
uzoefu na masuala ya michezo na uongozi.
Afisa Mawasiliano mpya wa
Yanga Kizuguto ameishukuru Kamati ya Utendaji kwa kumuamini na kumpa
nafasi hiyo ambapo amomba ushirikiano kwa vyombo ya habari, uongozi na
wanachama katika kufanikisha malengo ya kuifanya klabu ya Yanga kwenda
mbele zaidi. (Source:http://www.youngafricans.co.tz)
No comments:
Post a Comment