Ombi la uhamisho wa usajili wa mkopo nje ya dirisha la usajili la Didier Drogba limekataliwa na FIFA.
Gwiji huyo wa zamani wa The Blues amekuwa akihusishwa na kurudi Chelsea kwa uhamisho wa mkopo wa muda mfupi wakati wa mapumziko ya ligi kuu ya China lakini FIFA leo wamekataa maombi ya nahodha huyo wa Ivory Coast.
Shirikisho hilo la soka duniani lilisema kwenye taarifa yake: "Tunathibitisha kwamba tulipokea maombi ya mchezaji Didier Drogba kuomba ruhusa ya kusajiliwa nje ya kipindi cha usajili kwa mkopo.
"FIFA imemualifu mchezaji juu ya kanuni zilizopo.....kwamba wachezaji wanaweza kusajiliwa katika vipindi viwili tu vya mwaka vya usajili vilivyowekwa na vyama vya soka."
FIFA ilisema ingewezekana tu kwa Drogba kuhama kama asingekuwa na mkataba na kalbu nyingine ndio angeweza kusajiliwa kwa wakati ulio nje ya dirisha la usajili.
Drogba alikuwa anahitaji kupata sehemu ya kuendelea kujifua kabla ya kwenda kwenye michuano ya mataifa huru ya Afrika 2013.
No comments:
Post a Comment