Search This Blog

Monday, November 12, 2012

KIM POULSEN AUSIFIA UWANJA WA CCM KIRUMBA.


 Na Albert  G. Sengo.

KOCHA wa Timu ya Taifa Stars Kim Poulsen ameusifu uwanja wa CCM kirumba na kusema kwamba ni moja ya viwanja bora nchini na wachezaji wake watautumia vyema kuibuka na ushindi dhidi ya Harambee Star ya Kenya unaotaraji kuchezwa kwenye dimba hilo siku ya Jumatano ukiwa ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa kuendana na kalenda ya FIFA uliopangwa kufanyika Mkoani Mwanza na shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.
Akizungumza baada ya mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Kirumba asubuhi ya leo ameeleza kuwa mchezo wa Taifa Stars na Harambee Star utakuwa mgumu kulingana na kila timu kujianda na maandalizi ya mchezo huo huku ikizingatiwa kuwa wapinzani wao Harambee star inao wachezaji pia wanaocheza nchini Kenya na nchi za Ulaya hivyo kufanya upinzani kuwa mkali pamoja na ujio wa wachezaji wetu Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaokiputa  TP Mazembe umeongeza molali kwa wachezaji.
Poulsen amesema kuwa baada ya mchezo wa jumatano timu hiyo ya taifa itaendelea na kambi yake Jijini Mwanza kujiandaa na michuano ya Challenge Cup inayotarajia kuanza hivi karibuni nchini Uganda kwa kushirikisha Mataifa ya nchi za Ukanda wa Afrika mashariki na kati zitachuana .
Wachezaji wote wanamolali na wanaonekana kushirikiana vyema na nidhamu kwenye kambi ni nzuri na  matumaini ya kushinda mchezo huo kutokana na ushirikiano ulionyeshwa na vionozi wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA),TFF na wadau wengine wa michezo kuanzia mapokezi na ubora wa Kambi ya timu iliyopo katika Hoteli ya La-Kairo umewapa matumaini wachezaji kufanya vizuri na kucheza kufa na kupona ili kuibuka na ushindi wa mechi hiyo ya kimataifa.

Nahodha wa Stars Juma Kaseja akizungumzia kambi na mazoezi ya timu hiyo Jijini Mwanza amesema kuwa wachezaji wamefurahia mapokezi na mazoezi yanaonyesha kila mchezaji na molali ukizingatia wote ni wachezaji waliochaguliwa kutoka timu zinazoshiriki Ligi kuu ya Vodacom hivyo niwazuri kilichobaki ni mwalimu kutuunganisha kucheza kwa mfumo atakaoutumia jumatano.

Kaseja ameongeza kuwa wachezaji wote wanatambua wajibu wao hivyo kila mchezaji ametambua thamani yake ya kuchaguliwa kuchezea timu ya taifa hivyo jukumu kubwa ni kuitumikia timu hii kwa moyo na uzalendo kwavile ni timu ya watanzania wote hivyo kufanya vizuri kwa timu hii pia kutatuongezea alama FIFA kwa vile ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki tunawaahidi watanzania kuwa hatutawaangusha bali wajitokeze kwa wingi kuja kutushangilia ndani ya dimba la CCM Kirumba Jumatano na kwamba Harambee hawatatoka na ushindi.

No comments:

Post a Comment