October 29th 2002, Andres Iniesta aliichezea Barcelona kwa mara ya kwanza, katika mechi ya Champions league ugenini dhidi ya Bruges.
Hii ndio historia yake ya matukio muhimu katika kipindi hiki cha miaka 10 akiwa na Barcelona na kuweza kujitengeneza nafasi ndani ya kikosi na kupata mafanikio makubwa.
Hii ndio historia yake ya matukio muhimu katika kipindi hiki cha miaka 10 akiwa na Barcelona na kuweza kujitengeneza nafasi ndani ya kikosi na kupata mafanikio makubwa.
SIKU YA KWANZA MAZOEZINI
5th February 2001. “Ni kumbukumbu nzuri sana – Nilikuwa naonekana mnene kiasi! Hii ndio siku ya kwanza nimekutana na watu ambao ni mashujaa wangu, ilikuwa ni siku nzuri sana kwangu, nilipoitwa nilishindwa kuamini. Ningependa kumshukuru Serra Ferrer kwa nafasi aliyonipa kwa kweli imenifanya kuwa hapa nilipo sasa.
MECHI YA KWANZA VS BRUGES
29th October 2002. “Nilijisikia vizuri sana siku hii." Kulikuwa na wachezaji wengi wa timu B walioenda kwenye safari ile, kwa sababu tulikuwa tumeshapita kwenda raundi ya pili. Ni ndoto ya kila mchezaji kinda kucheza mechi yake ya kwanza na mie namshukuru sana Van Gal kwa nafasi aliyonipa.
MECHI YA KWANZA UWANJA WA NYUMBANI NOU CAMP
5th January 2003. “Timu ilikuwa imebadilika sana kiukweli haukuwa mchezo mwepesi.". Nilikuwa na hisia kama zile dhidi ya Bruges - nililelewa pale na kucheza mechi ya kwanza Camp Nou kilikuwa kitu muhimu sana. Ulikuwa mchezo dhidi ya Recre na tukashinda kirahisi 3-0."
GOLI MUHIMU DHIDI YA VALLADOLID
11th April 2004. “Moja ya picha zangu bora. Nina mahusiano mazuri na Valdes - ni rafiki yangu mkubwa sana. Alikuwa na furaha sana na akanikimbilia kutoka golini kwake kuja kushangilia goli na mimi. Lilikuwa goli tatu dhidi ya WAPINZANI WETU."
USHINDI WA CHAMPIONS LEAGUE JIJINI PARIS
17th May 2006. “Lilikuwa kombe la kwanza kubwa kushinda. Nina kumbukumbu nzuri sana kuhusu mechi hasa kwenye kipindi cha pili nilipoingia kuchukua nafasi ya Edmilson. Ni kombe muhimu sana na kwa bahati nzuri haikuwa mara ya mwisho kushinda kombe hilo.
GOAL! MUHIMU DHIDI YA CHELSEA
6th May 2006. “Kumbukumbu muhimu, kitu ambacho siku zote nitakikumbuka maisha yangu yote. Ulikuwa ni wakati ambao kulitatikana maajabu ili kuiokoa timu yangu na kwa uwezo wa mungu bahati ya kufanya hivyo ikaja upande wangu nikafunga goli lile na kuipeleka timu yangu fainali ya Champions league.'
BARÇA’S BALLON D’OR
6th December 2010. “Ilikuwa ndio siku ambayo walitangaza kwamba sisi watatu ndio tulikuwa tumeingia fainali ya kushindania tuzo ya Ballon d'Or. Sidhani kama hilo litatokea tena. Kilikuwa kitu tofauti sio tu kwa wachezaji bali kwa timu nzima kwa sababu ilikuwa ndio timu pekee iliyoweza kufanya hivyo."
A SPECIAL DEDICATION
6th April 2011. “Ulikuwa ni mchezo wa Champions League dhidi ya Shaktar na nikafunga goli katika dakika ya kwanza. Picha hii ilipigwa siku 2 baada ya mtoto wangu Valeria kuzaliwa. Ni mtu ambaye amebadilisha maisha yangu kabisa na kunifanya kuwa na furaha sana, pia amenifanya nielewe vitu vingi katika maono mapya. "
TUZO YA UEFA
30th August 2012. “Nipo na familia yangu, lakini baba yangu hakuwepo pale kwa sababu hapendi kupanda ndege. Japokuwa siku zote huwa karibu na mie, hata kama hayupo pale kimwili. Sichezi mpira kushinda tuzo binafsi - hiyo ni sehemu ndogo sana katika soka. Kushindanishwa na wachezaji akama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ni zawadi tosha."
No comments:
Post a Comment