Search This Blog

Monday, October 22, 2012

MFUMO WA UZUIAJI UTAWAGHARIMU BARCELONA MSIMU HUU

Hii post inaweza ikawa imechelewa kidogo, lakini ina ukweli mkubwa ndani yake juu ya mfumo wa ufundishaji kwa upande wa uzuiaji wa Tito Vilanova, ambaye aliteuliwa kuwa mrithi wa Pep Guardiola ili aweze kuendeleza filosofia ya soka walilokuwa wakilifundisha kwa pamoja na Pep Guardiola na kupata mafaniko makubwa kwa miaka kadhaa iliyopita.
Wakati ni kweli kwamba mfumo wa Barca haujabadilika sana, lakini ni kweli pia kwamba Vilanova ameutelekeza  mfumo wa mabeki watatu (isipokuwa wakati timu yake inapokuwa nyuma). 
Tuangalie mifano ya picha namna safu ya ulinzi ya Barcelona ilivyokuwa katika mechi dhidi ya Real Madrid  October 7.
  • Real Madrid goal #1

Real Madrid walikuwa wanafanikiwa katika kupeleka mpira kutoka upande mmoja mwingine hadi mwingine, kupitia mipira mirefu ya Xabi Alonso. Mpira hapa ulitoka upande wa kulia kwenda kushoto, huku Ozil akiurudisha kati. Huku kukiwa na presha ndogo katika kuzuia, mawinga wa Barcelona wanakuwa hawana uhakika nini cha kufanya wanapokuwa hawana mpira na mara nyingi wanakuwa wanajishahau kuzuia. Katika kesi hii, kuna wachezaji watano wa Madrid katika box dhidi ya wachezaji walio idadi sawa ya mabeki wa Barca. Tazama namna Ronaldo(aliye na kiduara cha blue) ameachwa akiwa sambamba na Dani Alves huku kukiwa na nafasi kubwa ya  kuweza kufanya utundu wake kwenye duara kubwa lenye kivuli.


Na pale Ozil anapompasia Benzema, mmoja wa mabeki wa kati anamfuata Benzema, kama anavyopaswa, na Dani Alves(kwenye kiduara cha Orange) anasitasita kwenda kumkaba Benzema au aendelee kumuangalia Ronaldo. Kwa mara nyingine tena, winga wa Barca wa upande wa kulia haonekani kwenye eneo hili pia Xavi na Fabregas waliocheza viungo wa katika mechi hii hawaonekani kusaidia katika box.

Kusita mara moja tu kwa Dani Alves kunamtosha Ronaldo kumpita mbrazil huyo aliyekwenye kiboksi cha orange na kuweza kufunga bao kwa shuti la mguuu wa kushoto.
  • Real Madrid goal #2

Kwa goli la pili Real Madrid, kulikuwa na kuna ishu nyingine katika kujipanga. Barcelona wamekuwa tofauti na siku za nyuma wanapoteza mipira hovyo hasa katika mechi kubwa na ngumu. Hapa kwa mara nyingine Barca walipoteza mpira na timu ikachukua muda mrefu kuweza kurudi shepu ya kuzuia. Eneo la kati (Lenye kivuli) halina ulinzi na beki wa kulia hayupo katikati ya goli na mtu anayemlinda kama anavyopaswa, huku Ozil akiwa katika eneo la kati pekee yake.

Huku mmoja wa mabeki akija kukutana na Ozil, Ronaldo anaingia kwa kasi kwenye eneo la hatari la Barca na kumpita beki wa kulia. Huku akiwa hana presha kutoka viungo wa Barca, Ozil ana;iga pasi safi na mtego wa offside sio kikwazo kwa spidi ya Ronaldo na movement za akili, anaingia ndania anipokea pasi ya Ozil na kuwaliza Barca. 
  • HITIMISHO
Pamoja na kuanza vizuri msimu mpaka kufika sasa, kiwango cha Barcelona bado hakijatisha kama siku za nyuma Umiliki wao wa mpira umekuwa sio mkubwa kwa mara kadhaa, lakini muhimu zaidi mfumo wao wa uzuiaji sio sahihi. Uharaka wa kukaba baada ya kupoteza mpira sio kama ule waliokuwa nao kipindi cha nyuma, pamoja na hilo kubadilika mfumo wa mzima wa kuzuia na kujipanga hakujabadilika sana kulingana na kasi yao ya kurudi kukaba wanapokuwa wanashambuliwa, hivyo mwishowe wamekjikuta wanaruhusu sana kuguswa kwa nyavu zao. Mfano mwingine mzuri ni mechi ya juzi dhidi ya Deportivo La Coruna iliyoisha kwa ushndi finyu wa 5-.

No comments:

Post a Comment