Mshambuliaji wa zamani Barcelona Henrik Larsson amempigia chapuo mchezaji mwenzie wa zamani Xavi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya mwaka huu baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwaenye timu ya taifa na klabu yake ya Barcelona.
Xavi, 32, ambaye alishiriki kikamilifu katika kampeni ya mafanikio ya Spain katika Euro 2012, na Larsson, ambaye aliichezea Barca kuanzia mwaka 2004 mpaka 2006, anahisi Xavi anastahili kupata tuzo hiyo muda huu kutokana na kiwango chake kizuri kwa muda mrefu.
"Lione Mess na Ronaldo ni wachezaji bora duniani, japokuwa Xavi anastahili kushinda zawadi hii kwa sababu amekuwa kiungo mzuri na mwenye mafanikio.
"Ingawa nadhani itakuwa ngumu kwa sababu amefunga mabao machache kulinganisha na Ronaldo na Messi,"alisema Larsson.
No comments:
Post a Comment