- Timu imara na bora hujengwa kuanzia katika idara ya ulinzi kisha idara nyingine kufuatia. Hujengaji wa timu inatakiwa umakini wa hali ya juu, hasa kama timu yenyewe itakuwa inakabiliwa na michezo ya Kimataifa. Timu ya Azam FC, ambayo itaiwakilisha Tanzani Bara katika michuano ya Kombe la Shirikisho hapo mwakani, ni timu ambayo inachipukia vizuri katika soka la Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Timu hii ina mkusanyiko wa wachezaji wanaojituma na bora katika ligi kuu yetu. Lakini mchezo wao dhidi ya Simba, jumamosi, iliyopita wanaweza kuuchukulia kama funzo kutokana na safu yao ya ulinzi inavyoweza kujilinda katika michezo mikubwa.
- Jana tumetoka kujifunza kitu muhimu kuhusiana na timu imara inavyoweza kuutumia ukuta wake kutwaa mataji, wakati mashabiki wengi wa Chelsea katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati wakiamini kukosekana kwa nahodha wao John Terry si pengo kubwa, wale wa London walikuwa tofauti sana na wengi waliokuwa nje ya nchi hiyo, walijiuliza na kukosa majibu kuhusiana na mlinzi gani kati ya David Luiz na Garry Cahill ambaye ataweza kumbana mshambuliaji Robin Van Persie wa Manchester United. Walizijua sifa za Terry za kujitolea, kutokata tamaa, na namna anavyoweza kujitawala yeye mchezoni na kuwaongoza wenzake katia safu ya ulinzi. Uchezaji wa mlinzi kama Terry ni tofauti kabisa na Luiz au Cahill, Terry hucheza kama mlinzi hasa wa mwisho na si mlinzi anayependa kuona mipira ikizagaa hovyo katika maeneo yao ya hatari, wakati walinzi kama Luiz na Cahill wakihitaji kujiimarisha zaidi kikosi hapo, bado wanaonekana ni walinzi wanaopendelea zaidi kuuchezea mpira hata wakiwa katika maeneo yao ya hatari. Tofauti yao inaanzia hapo.
- Mabeki hawa wanacheza msimu wa pili sasa wakiwa kama walinzi pacha, lakini bado hawajaweza kujitofautisha na uchezaji wa mabeki pacha wa zamani wa Simba, Kelvin Yondan na Juma Nyosso, wanacheza kwa papara sana na hawajui namna ya kubadilisha nafasi wakati mmoja akitakiwa kucheza kama namba nne na mwingine mlinzi wa mwisho, kwa muda sasa wameonesha hawawezi kuipaisha timu yao zaidi ya mahali inapofikia sasa. Wanashindwa kufanya vizuri sababu wote ni walinzi ambao kimsingi ni wakabaji na hakuna mwenye uwezo wa kucheza kama ' libero'.
Wakati timu inashambulia, hudondosha mipira yote inayoingia katika eneo la hatari. Namba tano anayecheza kwa mtindo huu huiweka timu yake salama zaidi kuliko yule anayetaka ' kuua kila mpira na kupiga chenga au kufanya kitu chochote' cha kiufundi akiwa na mpira katika maeneo yake ya hatari. Namba tano mzuri na anayetakiwa katika soka la sasa, ni muhimu zaidi kwake kuwa na sifa ya kuwapanga wenzake kila walipo wapinzani wake. Sifa nyingine ya namba tano wa kisasa ni yule ambaye anaweza kuanzisha pasi ' laini' kwa ama viungo au walinzi wenzake wa pembeni. Mlinzi wa mwisho ni lazima awe na nguvu, maarifa ya kucheza na kuipanga vizuri ngome yake, lakini pia anatakiwa kuwa na uwezo wa kujitegemea yeye kwanza, anatakiwa kujituma zaidi ya wachezaji wote kikosini. Namba tano mzuri anatakiwa pia kuwa na nguvu ya kuruka juu na kuondoa mipira yoyote ya hatari hasa ile ya kona na krosi. Kila afanyacho ni lazima kiwe sahihi. Ku 'clear' mipira yote inayoingizwa katika maeneo yao ya hatari na awe mwepesi pia wa kuusoma mchezo mara tu baada ya kuanza kwani baada ya golikipa, yeye ndiye anayeitazama timu vizuri zaidi.
Inawezekana mlinzi wa Simba, Paschal Ochieng hajaweza kuwaridhisha wapenzi wa timu yake kutokana na mchezo wake hadi sasa. Lakini wakati Watanzania wengi tukiamini kuwa mlinzi mahiri ni yule anayekimbia sana Ochieng yeye hucheza kama, Per Mertesacker wa Arsenal, hana spidi sana, lakini ni mlinzi anayeweza kukimbia na mshambuaji yeyote yule na kumzidi maarifa, anacheza zaidi katika maeneo yake kama , mlinzi wa mwisho. Ochieng ni mwepesi wa kuondosha mipira ambayo huzagaa katika eneo lao la hatari na ni mwepesi wa kuituliza timu inapokuwa inashambuliwa. Ana piga pasi nzuri kwa walinzi wake wa pembeni au viungo wake ni mtuilivu na anayepanga vyema beki yake/
Ukimtazama, Mbuyu Twite wa Yanga, yeye amejipambanua kama mchezaji wa kimataifa kwa miaka sita sasa na amekuwa akitumia nguvu na akili kila anapokuwa na mpira katika himaya yake. Mbuyu ana uwezo wa kucheza kama mlinzi wa pembeni kwa usahihi na vilevile ana uwezo wa kucheza kama mlinzi wa kati kwa usahihi mara kumi zaidi ya anapocheza nafasi nyingine. Ni mlinzi ambaye hajali sana kupiga chenga ili aonekane anajua chenga, bali yeye hutimiza jukumu la namba tano kwa kuondosha kwa usahihi mipira yote,
Kwa upande wa Owino yeye anaweza kuwa bora zaidi ya wawili hawa kwa sababu ana vitu ambavyo vinamfanya kuonekana kama namba nne aliyekamilika au namba tao mwenye uwezo wa juu zaidi katika ligi ya Tanzania, lakini wakati Azam FC wakipepesuka katika idara ya ulinzi dhidi ya Simba, wikiendi iliyopita walihitaji kuwa na sentahafu mwenye sifa kama za sentahafu ambaye alikuwa nje kabisa ya uwanja, OWINO. Mganda huyu ameshaonesha alivyo mlinzi mahiri katika misimu yake miwili aliyokuwa akiichezea Simba, lakini bado hajapata muda zaidi wa kuaminiwa na makocha wa Azam FC, lakini wakija siku kutambua thamani na uwezo wake bila shaka wanaweza kuwa wamechelewa sana, ni wakati wa Azam kuanza kumtumia Owino kwani, Said Mourad na Aggrey Morris wote ni walinzi wa aina moja, ni kama walivyokuwa wakicheza Juma Nyosso na Kelvin Yondan wakati ule wapo Simba.
nimeelewa kitu kimoja hapa, you wanted to talk chelsea, man u game through azam! do you remember chelsea, arsenal last season the five two game van persie scoring a hatrick and one goal being the obvious error from terry?
ReplyDeleteHao walinzi wameanza kuwa wabovu baada ya kufungwa na Simba tu...walinzi wanapimwa kwa record ya timu katika mechi za ligi...Azam ndio imeanza kufungwa na Simba juzi toka ligi ilipoanza na Aggrey na Morad ndio wamecheza almost mechi zote unasemaje leo wabovu....
ReplyDeleteNimeupenda uchambuzi wako lakini Owino wa Simba (miaka mitatu iliyopita) sio Owino wa leo hii (2012) namaanisha Simba ina mapungufu kwenye safu yao ya ulinzi lakini huwezi kusema benchi la ufundi la simba linatakiwa kuanza kumtumia Victor Costa eti kwa sababu alikuwa mchezaji mzuri mwaka 2002
ReplyDeleteAbdul ally yuko sahihi ni kama vile ulivyomsifia Blackberry hakuishi kama matarajio yako akatimuliwa kwa kutokua na kiwango.
ReplyDeleteYou really make it seem so easy with your presentation but I find this matter to be really something which I think I would never understand.
ReplyDeleteIt seems too complex and extremely broad for me. I'm looking forward for your next
post, I'll try to get the hang of it!|
My blog: program pit 2013 (Roadbiker.Student.Utwente.nl)