Mbuyu Twite na Kocha Tom Saintfiet |
Wiki iliyopita klabu ya Yanga ilimtimua kazi kocha Tom Saintfiet baada ya kuifundisha timu kwa takribani siku 80. Sababu kubwa iliyopelekea kocha huyo kupoteza kazi yake kwa mujibu wa viongozi wa Yanga ni kutofautiana sera za namna ya kuiendesha timu hiyo.
Kabla ya kocha huyo hajafungasha virago Sports Bar ya Clouds TV ilifanikiwa kufanya nae mahojiano kuhusu mambo yalivyoenda ndani ya klabu hiyo na hivi ndivyo alivyotiririka kocha huyo kutoka Ubelgiji ambaye amefanikiwa kuipa Yanga ubingwa wa Kagame.
KUTOFAUTIANA SERA NA MAWAZO NA UONGOZI
"Mimi ni kocha mzuri na mweledi sana - muda mwingine nakuwa mweledi sana kwa watu ninaofanya nao kazi. Ninakuwa nahitaji zaidi ubora kutoka kwenye klabu ninayofanya nayo kazi.
"Nilikuja Tanzania kushinda na kuwa bingwa - lakini pia kuongoza na kuhakikisha soka la hapa linaendelea mbele kwenye ngazi za juu zaidi.
"Nina mahitaji kadhaa ninayotaka kutoka kwa klabu - lakini viongozi wa klabu wamekuwa na mawazo mgando yale yale ya kila siku kuhusu u-proffessionalism katika utendaji wa kazi.
"Kuna maamuzi mengi mengi yamekuwa yakichukuliwa bila mie kuhusishwa wala kutoa ushauri wowote wa kiufundi - jambo lilipelekea kuwepo kwa kutokuelewana."
NI MAMBO GANI AMBAYO YALIKUWA YANAFANYIKA BILA WEWE KUFAHAMU?
"Sitaki kuyazungumzia kiundani sana, lakini kwa mfano kuna baadhi ya usajili wa wachezaji uliuwa unafanyika bila mie kufahamu chochote wala kuombwa ushauri kama mkuu wa benchi la ufundi kama nilikuwa nawahitaji wachezaji hao ama vipi. Pia kulikuwa kuna mambo ya kambi ya timu. Kwa kifupi haikuwa sawa kuchukua maamuzi hasa ya kiufundi bila mwalimu kuhusishwa."
UNAUZUNGUMZIAJE USAJILI WA MBUYU TWITE?
Mbuyu Twite ni mchezaji mzuri sana ambaye hakuwa kwenye listi ya mahitaji yangu ya wachezaji. Pendekezo langu kwa uongozi lilikuwa ni kuletewa mshambuliaji wa ziada na nikawapa jina mtu ninayemtaka na nikadhani wapo tayari kwenye mazungumzo ya kumsajili lakini haikuwa hivyo - nikaja kuona kwenye vyombo vya habari juu ya usajili wa Mbuyu Twite bila mie kuambia wala kuulizwa chochote.
Twite ni mchezaji mzuri sikuwa na namhitaji kwenye timu, nafasi yake tayari kuna mabeki wa kati wanaocheza vizuri sana, Kelvin Yondani, Cannavaro, Ibrahim Job, Issa na Chuji Athumani Idi anaweza kucheza eneo hilo, kwa hiyo tayari nilikuwa machaguo mengi kwenye nafasi hiyo, Twite hakuwa na mahitaji yangu, lakini mchezaji mzuri."
No comments:
Post a Comment