Search This Blog

Wednesday, September 12, 2012

UKWELI UNAOFICHWA: HIVI NDIVYO MCHAKATO MZIMA WA KELVIN YONDANI ALIVYOIDHINISHWA KUICHEZEA YANGA NA KAMATI YA MGONGOLWA

Muda mchache uliopita Shirikisho la soka nchini TFF limetoa taarifa rasmi juu ya mchakato mzima na maamuzi yaliyochukuliwa katika kikao cha kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji juu ya mapingamizi yaliyowekwa na vilabu dhidi ya baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali za ligi kuu ya Tanzania bara.

Baada ya kuisoma taarifa ile ambayo kiuhalisia kuna sehemu imepotoshwa kwa maana kwamba au ukweli wa mambo yalivyoendeshwa mpaka kufikia maamuzi unajaribu kufichwa, hasa kwenye kipengele cha uamuzi wa pingamizi la mchezaji Kelvin Yondani.

Kwa taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba kikao cha kamati ya Sheria, maadili na hadhi za wachezaji kilichokutana jana kilihudhuriwa na wajumbe watano Lloyd Nchunga, Iman Madega, Ismail Aden Rage, Omar Gumbo, Hussein Mwamba pamoja na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwanasheria Alex Mgongolwa.

Katika kikao hicho wajumbe walijadiliana katika kuweza kutatua na kupata suluhisho la mchezaji Kelvin Yondani ambaye amesajiliwa na vilabu viwili vikubwa vya Simba na Yanga lakini wakashindwa kupata muafaka kwa njia ya majadiliano, ndipo wakaamua kutumia njia ambayo ipo nje ya kanuni kwa kuamua kupiga kura miongoni mwa wajumbe. Kura zikapigwa huku Rage, Gumbo, na Mwamba wakipiga kura Yondani aidhinishwe Simba huku kura za Iman Madega, Nchunga, na Mwenyekiti Mgongolwa zikitaka mchezaji huyo aidhinishwe kucheza Yanga. Kwa maana hiyo matokeo ya kura yakashindwa kuamua kesi. Lakini kwa kuwa mwenyekiti ana mamlaka makubwa na uwezo wa kupiga kura ya Veto basi akachukua jukumu hilo na kupiga kura akimuidhinisha Yondani aende Yanga.


Kiuhalisia na namna ya demokrasia ilivyo mtu mmoja hawezi kupiga kura mara mbili kwenye ushindani mmoja kwa sababu kutakuwa hakuna usawa. Hivyo haikuwa sahihi kwa Mwenyekiti kupiga kura mara mbili.

Lakini kabla ya kufikia yote haya, hakuna utaratibu wowote duniani kwenye masuala ya usajili unaolekeza ikitokea hali kama iliyopo kwa Yondani basi zipigwe kura. Kiuhlasia ilibidi sheria zilizopo zenye kuamua kesi kama hiyo zifuatwe. Inajulikana wazi kwamba ni kosa kwa mchezaji kusaini mkataba na timu mbili tofauti kwa wakati mmoja na adhabu zake zimeanishwa kabisa kwa klabu iliyocheza rafu na mchezaji mwenyewe. Na katika sheria hizo hakuna mahala kunapoelekeza uwepo wa upigaji kura kuamua kesi ya namna ya Yondani au Twitte.

Sawa basi hata kama kamati iliamua kutumia mfumo wa upigaji kura basi ungepaswa kuwa na usawa na sio kama ilivyotendeka. Haiwezekani mtu mmoja ambaye tayari ameshaonyesha yupo upande mmoja kati pande mbili zinazopingana tena zenye wajumbe sawa apewe nafasi ya kupiga kura mbili.

Lakini haikutakiwa jambo hili lifike kwenye hatua hii - sheria ziliwekwa na shirikisho la soka chini ya muongozo wa kanuni zinazoongoza soka zilibidi zifuatwe katika uamuzi wa mapingamizi haya ili kuweza kukomesha vitendo vya namna ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya soka letu.

11 comments:

  1. NGUGU ZANGU WAPENDA MICHEZO NI MTAZAMO WANGU KUWA TFF PAMOJA NA KAMATI YAKE YA MAADILI NA HADHI ZA WACHEZAJI WAMETUMWA KUUWA MCHEZO WA SOKA TANZANIA. NASEMA HIVI KWA SABABU MAAMUZI WANAYOTOA JUU YA PINGAMIZI ZILIZOTOLEWA ZINALENGA KUINUFAISHA TIMU YAO TFF a.k.a YANGA. HIVI WENZANGU MLISIKIA WAPI SHERIA ZINAAMRIWA KWA KUPIGA KURA? HIVI KWELI MTU ANAWEZA KUHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KUPIGIWA KURA JOPO LA MAJAJI KAMA ANAKOSA AU LA? MATOKEO YA UENDESHAJI WA MAMBO YA MPIRA KWA TFF YATASABABISHA MAUAJI KWA MASHABIKI KWA SABATU TU YA CHUKI ZINAZOPANDIKIZWA NA TFF KWA MASHABIKI KWA KUIBEBA TIMU YAO(YANGA) YAANI YALIYOTOKEA MISRI YATATOKEA TU TANZANIA HASA UHASAMA ULIOJENGWA KWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA. NI MAONI YANGU KUWA TFF IBADILISHE JINA NA IITWE YFF YAANI YOUNG FOOTBALL FEDELATION NA SIO TANZANIA FOOTBALL FEDELATION COZ WAKO PALE KWA LENGO LA KUIENDELEZA YOUNG AFRICANS NA SIO SOKA LA AFRIKA. WAMELITIA AIBU TAIFA AMBALO HATA DUNIA INATAMBUA KUWA NI KATI YA NCHI YENYE WANASHERIA MAHILI. NAOMBA WAPENDA SOKA WENZANGU TUINUSURU SOKA YA TANZANIA KWA KUITISHA MAANDAMANO NCHI NZIMA KUIONDO TFF a.k.a YFF NA MIMI NAJITOLEA KUZUNGUKA TANZANIA NZIMA KWA MANUFAA YA SOKA YETU TANZANIA NA NAANDAA WALAKA KUUSAMBAZA TANZANIA NZIMA KWA WAPENDA SOKA. NAOMBA KUWASILISHA. BY MKINGA C.J

    ReplyDelete
  2. Shafii acha kupotosha umma! acha kabisa! hata mauaji ya kimbari Rwanda 1994 yalisababishwa na watu WAONGO na watunga maneno ya UONGO kwa mapenzi yao binafsi.

    Ushauri:
    Acha kufanya mambo yanayokufarahisha nafsi yako! badala yake kuwa mkweli na itumikie jamii itakuheshimu la sivyo utaendelea KUDHARAULIWA na KUDALILISHWA!

    Hebu soma hapo chini we mwongo wewe!

    Mbuyu Twite
    Kwa mujibu wa Ibara ya 18(3) ya Kanuni za Hadhi na Uhamisho wa Wachezaji wa Kimataifa za FIFA, Yanga ilifuata taratibu zote katika kumsajili Mbuyu Twite, hivyo ni mchezaji wake halali. Hata hivyo, kwa vile Yanga imekiri kuwa mchezaji huyo alichukua dola 32,000 za Simba na kukiri kuzirejesha, kwa msingi wa kanuni ya Fair Play, Kamati imeipa Yanga siku 21 iwe imelipa fedha hizo Simba.
    Kelvin Yondani
    Kwa mujibu wa Ibara ya 44(3) ya Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za TFF, Yanga ilifuata taratibu zote katika kumsajili Kelvin Yondani, hivyo ni mchezaji wake halali.
    Kwa vile Simba imesema mchezaji huyo vilevile alisaini mkataba na klabu yao, imetakiwa kupitia mamlaka nyingine kuthibitisha hilo, na baada ya uthibitisho iwasilishe malalamiko yake kwenye Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, au mamlaka zozote za kisheria kwa mujibu wa madai/lalamiko husika.
    Alex Mgongolwa
    Mwenyekiti
    Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji

    ReplyDelete
  3. Hapa ndipo Watanzania tunajishusha wenyewe,. Hivi huyo mwenyekiti wa hiyo kamati ni mwanasheria kweli!!? Na kasomea sheria gani!!? Hivi unaacha kutumia taaluma yako then unatanguliza mapenzi binafsi katika maamuzi mazito kama haya!!!? Kuna haja kubwa sana ya mabadiliko katika mfumo wa soka letu,. Hata namna ambayo vilabu vyetu vya soka vibafanya usajili wake ni batili.. Hivi ni nchi gani duniani timu pinzani inamsajili mchezaji kwanza, then ndo inaenda kwenye timu aliyotoka mchezaji kutangaza ofa ya usajili!!!? Kwa mfano Alex Ferguson asingeweza kumalizana na Robin Van Persie then ndo aende kwa Wenger amwambie kwamba "eeh bwana eeh, yule mchezaji wako nshamchukua, we unataka nikupe shillingi ngapi!!?" kwanza atafungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi kirefu, even milele kabisa., System ya usajili bongo inatakiwa kubadilika ili kuepusha matatizo kama haya ya kamati za nidhamu zenye mapenzi binafsi,. Pia viongozi wetu wa soka wako pale kwaajili ya kuongoza soka la tanzania sio la timu fulani... TUBADILIKE

    ReplyDelete
  4. Jana Nilimsikia Alex Mgo. alikataa katakata kuwa maamuzi hayo yalizingatia kanuni. Hoja hapa ni mbili -- (1) Yondani alikuwa mchezaji huru kwa kuwa Simba haikusajili maboresho ya mkataba TFF au hawakufahamu na walifanya kimazoea tu, hivyo kutokujua sheria si utetezi (ignorance of law is not a defence)

    (2) Simba ilijaribu kuupeleka/kuusajili mkataba wa maboresho wa Yondani na TFF hawakuwajibika (wakawachenga), hiyo inaweza kuwa ni uzembe wa kiutendaji wa TFF, au labda watu wa TFF walijua tayari Yondani kesha haribu na wakaipendelea Yanga.

    kama yondani alisaini Simba na Simba hawakufanya mchakato wa kuhuisha mkataba kabla ya Miezi Sita kufikia kikomo cha mkataba basi Yondani ni Mwizi anapaswa kuwajibishwa kisheria, na kama simba walizembea basi wakubali uzembe na wasiwadanganye washabiki wao ili kulinda nafasi zao za uongozi, vile vile kama TFF waliletewa nakala ya maboresho ya mkataba wa yondani na wakazembea (Hawakuufanyia kazi ) wanapaswa kuwajibishwa pia.

    pendekezo, Mimi naona status za Mikataba ya Wachezaji ziwe zinawekwa kwenye website na wadau wote tuzione. Timu zote mbili (Simba na Yanga) wanapaswa kuadhibiwa kwa kufanya makosa ya kusajili mchezaji bila kupata status kwa Club (Simba wamefanya mara mbili kwa kipindi hiki cha usajili - yule kinda wa azam na Rendondo) na Yanga wamefanya (kama yondani hakuwa huru) kwa Yondani.

    Azam wangekomaa na kuwashtaki simba na si kutumia busara ingekuwa fundisho.

    Nwasilisha.

    ReplyDelete
  5. shaffii acha usanii huyo rage na gumbo kama walikubali kupiga kura basi hao ndio waliopindisha kanuni kama wangetataa kupiga kura ndio tungewashutumu viongoz wa TFF Rage anajua anachofanya aache kuwahadaa wanasimba

    ReplyDelete
  6. Mgongolwa pamoja na kamati yako yenye nia ya kuuwa soka Tanzania msijitetee kwa nia yenu ya makusudi kujenga chuki miongoni mwa watanzania wapenda soka.
    Usimtuhumu Saffii eti kaudanganya umma wakati ndicho mlichokifanya. Ninaamini na ninawasiwasi mkubwa wewe ni kati ya vilaza waliojiingiza kusomea sheria kwa kufuata mkumbo hasa pengine kwa kushawishiwa VIJISICHANA VYA VYUONI. Nina masikitiko makubwa kuona Mgongolwa mna nia ya kuuwa soka Tanzani. Ninaungana na MKINGA C.J mtoa maoni wa kwanza hapo juu kuiondoa TFF a.k.a YFF ili kuinusuru soka yetu. By NGWATINGWATI MAYUNGA wa MBEZI BEACH DSM

    ReplyDelete
  7. Lazima tukubali kua kuna ubabaishaji mkubwa ndani ya TFF, hapa suala sio usimba au uyanga..ukaiangalia jinsi mchakato mzima wa jinsi yale maapingamizi yanayozihusu simba na yanga yalivyoamuliwa inaonesha wazi kua hatuna chombo cha mpira kilicho serious. Kwa mfano issue ya Redondo kwenda Simba japo jana nilimsikia Mgongolwa akitoa maelezo ila sijaridhika na maelezo yake kbs. Redondo amefanya kitendo cha kihuni kwenda simba na kusema kua mkataba wake umeisha wakati sio kweli simba nao kwakua hawako serious badala ya kufuatilia wakamsajili, huo sio ukiukwaji wa kanuni? Hata kama Azam hatimae walikubaliana na Simba baadae haikua sahihi manake mda wa usajili ulikua ushapita japo Mgongolwa amekana hili. Issue ya Yondani ilivyokua handled pia ni uatata mtupu...Kwa mfano kama ni kweli issue ilikua simple kama ambavyo mgongolwa alijaribu kueleza jana nn kilichofanya wachelee kutoa maamuzi mda wote huo? kwann waliwakutanisha viongz wa simba na yanga ili wakubaliane? ni kanuni gani inayosema watu wakutane wakubaliane wakati ipo wazi kua kanuni hazikufuatwa? Mgongolwa anasema Yanga walifuata taratibu zote ktk kumsajili Yondani hivyo ni mchezaji wao halali, kama ni kweli kwanini ktk maamuzi yao kuna sehemu wanasema simba wathibitishe mkataba wao na Yondani kwa vyombo husika kisha wawasilishe malalamiko yao tena? what for? Je simba wakifanikiwa kuthibitisha kua walikua na mkataba halali na Yondani, kamati hii itatengua tena maamuzi yake wakati wameshadeclare wazi kua taratibu zilifuatwa kwakua Yondani alikua mchezaji huru/ tuache ushabiki tuliangalie hili suala objectively kama watu wa michezo...Nionavyo mm tatizo kubwa ni kamati hii kujaa watu wa simba na yanga, hakuna namna haki inaweza tendeka wakati wenyeviti wa simba na yanga ndo wana kamati na issues zilizopo mezani zinawahusu wao..haki huenda itatendeka kama ni suala ambalo si la simba au yanga...wangetakiwa wawepo watu ambao ni impartial wasio na uanachama wa timu yoyote na ambao wana uelewa wa sheria na kanuni za mpira..

    ReplyDelete
  8. Huyu Shaffih mara nyingi huwa anapenda sana kuiponda yanga na mara nyingine huwa anawasapoti simba. kuna siku alishasema kwa nini yanga wanamsajili Twite wakati tayari kuna Nadir na Yondan na aliyekuwa mwenzake Ally Mayai alimkata kauli yake na kumuuliza kuwa Man city ina striker wangapi akaanza kujing'atng'ata. halafu hata katika Blog yake habari za yanga anaandika kwa lengo ya kuikosoa tu ila angalia alivyoandika eti simba yayesha barafu za azam. lakini yanga hawana kelele. Jana ktk kipindi cha spoti extra aliuliza swali hilo ingawa hakuwa na uhakika kuwa eti maamuzi yalipatikana kwa njia ya kura na jamaa alikataa kwamba wao walitafsiri sheria na hata rage alisoma hizo sheria na anazifahamu. Blogs hii ni kwa ajili ya wasomaji wote tuache kuandika masuala ya unazi katika chombo hiki cha habari.

    ReplyDelete
  9. Ushauri wangu,hawa watu wanaoanzisha blog zinazohusu habari mbalimbali(siyo zile blog ambazo mtu anaweka taarifa zake binafsi)embu wasome kwanza taaluma ya uandishi wa habari ili wajue namna ya kuandika taarifa au habari.
    Ni hilo tu.

    ReplyDelete
  10. We shaffih leo wacha nikwambie ukweli.... Wewe umekurupukia hii fani ya uandishi wa habari pasipo kuwa na elimu ya maana,lakini sio kosa lako, kosa ni la serikali kujaza utitiri wa vyuo vya second floor ambapo wewe umesomea kile chuo cha second floor pale ilala lol.... Just Joking bwana mkubwa.... Sasa back to the issue ni kwamba Shaffih na timu yako nzima mnaendekeza unazi, nilibahatika kusikiliza interview yenu na mwenyekiti Mgongolwa kwa kweli mlichokuwa mnakifanya ni ubabaishaji mkubwa kwenye tasnia hii ya habari, huwezi ukawa unamuhoji mtu kitu ambacho amekuwa anakikanusha mara tatu lakini still unakomaa kuuliza hilo hilo hivi mtapata wapi weledi wa kufanya kazi zenu kitaaluma? Mimi nina uhakika kabisaa kama kungekuwa na issue kama hiyo walahi wajumbe wenu wasingekaa kimya haswa mwenyekiti wenu Rage asingeweza kukaa kimya lazima angeutangazia uma wa wanamichezo kuelezea hiyo style iliyotumika kuwabariki hao wachezaje kwenda Yanga, punguza ubabaishaji kaka maana hata wakati mwengine unajaribu kutoa news kwenye INTERNET lakini still unakuja kuchapia chapia kwenye kipindi chako hapo, kama tunataka maendeleo kwenye tsnia hii ya mpira basi lazima tuwe na tabia ya kufuta kanuni zinavyosema na si kutaka kanuni zitufuate sisi...
    Mdau

    ReplyDelete
  11. Shafii shule ni muhimu! usichanganye hisia na kazi,utashindwa.

    ReplyDelete