Jorge Mendes ni mmoja ya watu wenye nguvu sana katika ulimwengu wa soka. Na bado watu wengi hawamfahamu kiundani.
Ni namna gani Jorge Mendes amekuwa na nguvu kwenye ulimwengu wa soka.
Songimbingo jipya limeibuka na suala la Cristiano Ronaldo. Ripoti zinasema kwamba chanzo ni kukosa kwake tuzo ya mchezaji bora wa ulaya baada ya mchezaji huyo kukaririwa akisema hana furaha. Lakini upande mwingine inaonekana kama suala hilo linahusu masuala ya fedha; Ronaldo anataka mkataba wenye maslahi zaidi kwa mchango mkubwa anaoutoa kwa Real Madrid. Hili suala linaonekana lina mkono wa mmoja ya watu wenye nguvu sana kwenye ulimwengu wa soka. Mwanaume asiyejulikana na mashabiki wengi, lakini ni maarufu sana kwa wachezaji wakubwa wa dunia na wamiliki wa timu.; Jorge Mendes.
Unataka mshahara mkubwa? Fedha nyingi kwenye uhamisho? Jorge Mendes ndio mwanaume anayeimudu hiyo kazi hiyo. Jorge Mendes ni wakala wa soka raia wa Ureno, wakala wa mmoja ya makocha bora wa soka Jose Mourinho, wakala wa mmoja wa wachezaji bora duniani Cristiano Ronaldo na wachezaji wengi wa hadhi ya juu barani ulaya. Katika michuano ya Euro iliyoisha hivi karibuni, wachezaji 15 kati ya 22 wa kikosi cha Ureno walikuwa wakiwakilishwa na Mendes.
Katika miaka miwili iliyopita Mendes alipokea amepokea tuzo mara mbili tuzo ya wakala bora inayotolewa na Globe Soccer Awards. Kampuni yake ya Gestifute International inaingiza $200 million kwa mwaka. Mendes ni master wa kufanikisha madili makubwa ya usajili hasa kwa wachezaji wa kibrazil na kireno, lakini ni wapi mwanaume huyu anapotokea? Unapogundua kwamba ni mwanasoka aliyefeli na kuamua kuwa mmiliki wa klabu ya usiku, safari yake ya kuja kuwa wakala bora wa soka inasisimua.
Soka imekuja kuwa biashara nzuri mno, jukumu la mawakala limezidi kuwa na umuhimu mkubwa huku muda mwingine likiwasumbua sana makocha na vilabu. Vitendo vya kutishia vilabu ili kuongezewa mishahara au kutishia kuondoka vimeshaanza kuwa vya kawaida kutoka kwa mawakala ambao nia yao ni kuendelea kutengeneza fedha nyingi kupitia wateja wao. Imetokea kwa takribani miaka 10 iliyopita ikiwa mchezaji anataka kuondoka kwenye klabu, Mendes ndio mtu anayepigia simu kushughulikia dili hilo.
ALIANZAJE UWAKALA WA SOKA
Ilitokea siku moja Mendes akakutana na golikipa Nuno Espirito Santo mwaka 1996, ambaye mwanzoni alikuwa akiichezea Vitoria Gulimaraes. Santo alitaka kuhamia Porto lakini kutokana na upinzani uliokuwepo baina ya vilabu uhamisho huo ulikuwa hauwezekani. Mendes akiwa mmiliki wa klabu ya usiku wakati huo akizungumza na Santo na kumuuza Deportivo La Curuna. Lakini hii ilikuwa njia tu ya kumruhusu Santo aweze kufanikisha ndoto yake ya kwenda Porto.
Baada ya kukamilisha dili hilo, akahamia kabisa kwenye biashara hiyo ya uwakala. Mahusiano yake na Deportivo yakakua na alikuwa ndio mtua mbaye alifanikisha uhamisho wa mshambuliaji wa kireno Pauleta kutoka Salamanca kwenda Deportivo mwaka 1998.
Mendes akazidi kukua na kupata sifa, akamwakilisha Costinha na kafanikiwa kumhamisha kwenda AS Monaco na akafanikiwa kumhamisha Capucho kwenda Porto kutoka Guimarease. Milango ikaanza kufunguka na alikuwa akifanya maamuzi sahihi na muhimu zaidi alikuwa anategeneza mahusiano mazuri na watu sahihi kwenye biashara yake.
Huku sifa yake ikizidi kukua kukatokea upinzani wa kikazi kati yake na wakala mwingine aliyekuwa ana nguvu sana kwa wakati huo Jose Veiga ambaye alikuwa akiwawakilisha wachezaji wenye majina makubwa kama Figo, Joao Pinto, Mario Jardel, na Zidane. Mwaka 2002 mawakala hawa wawili waligombana sana baada ya Mendes kutaka kumchukua Figo kutoka Veiga.
Ingawa hakufanikiwa kwa Figo, Mendes aliweza kuwachukua Ricardo Quaresma na Ricardo Carvalho kutoka Viega. Hili liliwezekana kwa sababu aliweza kutengeneza mahusiano mazuri na Raisi wa FC Porto Pinto da Costa, uhusiano ambao ulimuwezesha Mendes na kampuni yake kwenda hatu nyingine mbele. Mendes akapewa dili ya kuwawakilisha wachezaji wakubwa wa Porto, hali ambayo ipo mpaka leo.
Mwaka 2002/03 Mendes alifanikisha dili kubwa la Jorge Andreade alipojjiunga na Coruna na Hugo Viana alipojiunga na Newcastle. Sifa ya Mendes nchini Spain ikazidi kukua.
KAKA WA CRISTIANO RONALDO
Wakati huo huo Mendes akatengeneza uhusiano wa kindugu na mchezaji kinda wa kireno aliyeitwa Cristiano Ronaldo. Akiwa na miaka 17 Ronaldo alikuwa ajulikani nje ya Ureno. Lakini bado Mendes na Sporting Lisbon waliweza kumtangaza kibiashara barani ulaya hasa nchini England.
Story ya kwamba Cristiano Ronaldo hajulikani ilikuwa uongo. Kwa sababu tayari alishapelekwa kwenye vilabu kama Arsenal na Liverpool kwa kipindi chote cha mwaka 2002 na kwa mujibu wa mwandishi David Conn alikuwa amekaribia kusaini kujiunga na Arsenal. Ingawa katika mechi ya kirafiki kati ya United na Sporting, ambapo aliwapeleka puta wachezaji watu wazima wa United na story ya kuwa kitokeo cha hapo wachezaji wale wakamshawishi kocha Sir Alex Ferguson amsajili ni uongo, kwa sababu dili lenyewe tayari lilikuwa limeshafanyika tena kwa fedha nyingi zaidi ya £5million walizo ofa Arsenal, United walitoa kiasi cha £12 million.
Dili la kumpeleka Ronaldo United lilifanikiwa zaidi kwa sababu ya fedha alizolipwa wakala Mendes. Suala la wakala kulipwa lilishawahi kuandikwa na kujadiliwa na BBC - kitendo ambacho kilimfanya Ferguson kutofanya interview na na kituo hicho kwa muda mrefu.
Kilichoonekana kufanyika ni kwamba Mendes alikuwa na mazungumzo marefu na CEO wa United David Gill ambaye alionganishwa nae na kocha msaidizi wa kipindi hicho Carlos Quieroz. Na kutoka kwenye dili la Ronaldo inaripotiwa Mendes alilipwa na United kiasi cha £1.2m.
Ingawa issue ya fedha za uhamisho ilileta maneno maneno sana, ukweli ni kwamba Ronaldo aliweza kweli kuimarika na kuwa mchezaji mkubwa duniani akiwa na United, na yeye, United na Mendes wote walifanya biashara nzuri sana wakati nyota huyo aliposajiliwa kwenda Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa zaidi ya £81 million mwaka 2009.
Mendes anaripotiwa kupkea 10% ya kila dili la uhamisho analokamilisha na hivyo uhamisho wa Ronaldo ulimuingizia Mendes kiasi cha £8million. Japokuwa sio Mendes, United wala Madrid waliothibitisha kwamba kuna fedha za ada ya uwakala zililipwa.
The Special One
Mendes akiwa na Jose Mourinho na Ronaldo katika moja ya mikutano yao |
Mwaka 2003 na 2004 Jose Mourinho alikuwa kwenye safari ya kuwa manager mwenye mafanikio akiwa na FC Porto kwenye mikono ya Jorge Mendes. Mafanikio ya Mourinho yalimfanya awe ndio kocha anayewindwa na vilabu kibao na Mendes akawa wakala wake.
Huku Chelsea ikiwa chini ya mmliki mpya aliyetaka kuitawala dunia ya soka, Roman Abramovich alitaka mtu ambaye alileta mafanikio kwenye klabu ya Porto. Mendes akafanikisha dilila kumpeleka The Special One Stamford Bridge na uhusiano mzuri baina ya Chelsea na Mendes ukazaliwa.
Wakati Mourinho alipowasili Stamford Bridge, alipenda kuwaleta baadhi ya wachezaji kutoka Porto. Akafanikiwa kuwachukua Thiago, Carvalho na Paul Ferreira kwa da ya pamoja ya £40million. Mendes alikuwa ndio wakala wa wachezaji wote watatu.
Mourinho akashinda makombe mfululizo kabla ya kuondoka baada ya kutoelewana na Abramovich. Lakini bado uhusiano wa Mendes na Chelseahaukushia pale. Alikuwa na mahusiano mazuri na Scolari na alikuwa ndio mtu aliyemshawishi Abramovich kumuajiri kocha huyo mbrazil ambaye baadae akaajiriwa na kuja Darajani pamoja na Deco na Bosingwa, wachezaji wengine wa Mendes.
*****************************************************************************
Uhusiano wake na United ulizidi kukua baada ya ujio wa wachezaji Nani na Anderson ambao wote walisajiliwa kutokana na maoni ya Carlos Quieroz. Sifa za Mendes zikazidi kukua na huku uhusiano wake na watu wenye nguvu kwenye soka ukizidi kuimarika.
Mendes na Anderson |
Kabla ya Mourinho kwenda Madrid, Pepe aliwasili Bernabeu naRonaldo akafuatia, katika kipindi cha mwaka 2007-2009 kwa ada ya jumla ya uhamisho ya £100 million. Tangu Mourinho afike pale amekuwa akiwashawishi mabosi zake kununua wachezaji walio chini ya Mendes. Usajili wa Di Maria na Coentrao kwa ada ya pamoja ya £50 million na Carvalho akaongezwa kwa ada ya £8million kutoka Chelsea, kwa maana hiyo Madrid kwa pamoja ilitumia kiasi cha £160million kuwasajili wachezaji wa walio chini ya Mendes, hivyo Gestifute - kampuni ya Jorge Mendes ilitengeneza asilimia 10 ya fedha zote walizotumia Madrid kuwasajili wachezaji walio chini yao.
Pamoja na mahusiano yake mazuri na United, Chelsea, na Madrid, uhusiano wake na Porto umeendelea kuwa na nguvu sana. Msimu uliopita Mendes alikuwa ndio kidume aliyefanikisha dili la Radamel Falcao kutoka Porto kwenye Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho wa ¢45million. Taarifa zinasema kwa hali ya uchumi ya Atletico ilivyo - Mendes alitoa nusu ya fedha za usajili huo. Ukiangalia kwa namna alivyofanikiwa Falcao kuanzia mwaka jana mpaka sasa msimu huu, thamani yake imeshapanda mpaka kufikia £60million+ bila swali, na huku matajiri wa vilabu vya Chelsea, Man City na PSG wakianza harakati za kutaka kumsaini - Mendes ameweka miguu juu tu akicheka na kusubiri malipo ya uwekezaji wake.
TUHUMA ZA WIZI WA WACHEZAJI
Uwezo wa Mendes katika kukamilisha madili ya uhamisho ni mzuri sana. Siku hizi mpaka wachezaji wachanga wanamfahamu kwamba ndio mtu anayeweza kufungua milango ambayo mawakala wengine wanashindwa.
Lakini mafanikio yake pia yamekumbwa na tuhuma za wizi wa wachezaji wa mawakala wengine. Ameshwahi kutuhumiwa na mawakala kadhaa juu ya tabia yake ya kuwalaghai na kuwaiba wachezaji na muda mfupi baadae nawauza kwa fedha nyingi - Wakala wa zamani wa Nani, Ana Almeida, alilalalamika kwamba mchezaji wake Nani aliamua kuachana nae na kujiunga na Mendes, na muda mfupi baadae akamuuza kwenda Manchester United - huku akiwa bado ana mkataba nae.
Lakini kubwa kabisa limekuja hivi karibuni katika uhamisho wa Bebekwenda United. Wakala wa Bebe, Goncalo Reis, anasema makataba wake na mchezaji ulikatishwa, kabla ya ghafla baadae Mendes akamchukua Bebe then ndani ya siku kadhaa baadae akakubaliana kumuuza mchezaji huyo kwa United kwa ada ya £7.5milion. Ripoti zinasema mteja wa Mendes - Carlos Quieroz alimpigia chapuo Bebe kwa Fergie na kumshawishi kocha huyo wa United kumsajili mchezaji bila hata kumuona.
Pamoja na yote hayo lakini watu walio karibu na Mendes wamekuwa wakimsapoti; Mourinho alimsifia Mendes na uwezo wake wa kutengeneza mahusiano mazuri na klabu na makocha, na kuwapa muongozo mzuri wachezaji kuheshimu mikataba na klabu zao. Huku Ronaldo akimuelezea wakala wake kuwa ni mtu safi na mpenda usawa.
SUALA LA CRISTIANO RONALDO
Wakati wachezaji wakiwa wanarudi kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kimataifa, vyombo vya habari vyote vilikuwa vinamzungumzia Ronaldo, huku ripoti zikisema kwamba anaweza kuondoka katika dirisha lijalo la usajili.
Ishu hii ya Ronaldo itawaamsha timu nyingi zikiwemo PSG, Man City, kwa ajli uwezekano wa upatikanaji wa Ronaldo, lakini hakuna kitakachotokea mpaka kipindi kijacho kiangazi. Mazungumzo ya mkataba mpya yamesimama kwa sababu imeripotiwa kwamba dili jipya litawagharimu £30m Madrid kwa ajili ya kodi.
Kitu kinachovutia kuhusu saga hili la Ronaldo ni kwamba wakati wa dirisha la usajili hivi karibuni Mendes alimwakilisha beki mbrazil Thiago Silva na kukamilisha uhamisho wake kutoka AC Milan kwenda PSG kwa ada ya £25m. Uhamisho huu unaweza ukawa mwanzo wa mahusiano kati ya PSG na Mendes.
Taarifa za kuaminika kutoka kwa watu waliokaribu na wakala huyo zinasema kwamba Mendes ndio mtu aliye nyumaya malalamiko ya Ronaldo dhidi ya Madrid. Mwanaume huyu aliyefanikisha uhamisho wa £80m kutoka United kuja Madrid anaona kabisa kuna upenyo wa kupiga hela nyingine kubwa. Sio jambo la kushangaza ikitokea kwamba wamiliki wa PSG wameshamhaidi kitu Mendes kwamba labda wapo tayari kulipa fedha nyingi ili kuwasajili wachezaji wakubwa. Cristiano Ronaldo atakuwa ndio mtu anayepewa kipaumbele kikubwa kama suala hilo litakuwa kweli.
Huku Mourinho akionekana naye yupo tayari kuondoka Madrid, Mendesanaonekana yupo tayari kufanikisha uhamisho mwingine mkubwa kwa klabu mpya ambazo zitakuwa tayari kulipa mkwanja mrefu. PSG ndio wanaonekana kuwa wanunuzi wazuri, mbele ya City ili kuvinunua vipaj vya Mourinho na Ronaldo.
Mpaka sasa kampuni ya Mendes inawawakilisha wachezaji 200 wengi wao wakiwa wanatoka nchini Brazil na Ureno. Kwa sasa Jorge ameweka nguvu nyingi katika kuwasaini wachezaji wadogo wenye uwezekano wa kuwa wakubwa mbeleni. 'Super Agent' Mendes anazidi kuwa mkubwa tu na nguvu nyingi kwenye soka kuliko hata baadhi ya vilabu.
Huyu ndio Jorge Mendes, kutoka kuwa mmiliki wa klabu ya usiku mpaka kuwa wakala bora na tajiri tena mwenye nguvu mno kwenye ulimwengu wa soka duniani. Kwa uwezo wake mkubwa wa kutengeneza marafiki na kufanya maamuzi bora amekuwa 'Super Agent' na kwa hali ya soko la usajili lilivyo tegemea kumuona na kumsikia sana na madili yake ya usajili katika miezi na miaka kadhaa ijayo.
HAYA NDIO BAADHI YA MADILI MAKUBWA YA USAJILI YA JORGE MENDES
Ronaldo £80m Man Utd - Real Madrid
Di Maria £25m Benfica - Real Madrid
Coentrao £25m Benfica - Real Madrid
Anderson £18m Porto - Man Utd
Pepe £20m Porto - Real Madrid
Danny £20m Dynamo - Zenit
Carvalho £20m Porto - Chelsea
Nani £18m Sporting - Man Utd
Bruno Alves £15m Porto - Zenit
Bosingwa £17m Porto - Chelsea
Ferreira £17m Porto - Chelsea
Simao £12m Benfica - Atletico Madrid
Manuel Fernandes £12m Benfica - Valencia 289
Deco £15m Porto - Barcelona
Tiago £12m Porto - Chelsea
Hugo Viana £8.5m Sporting - Newcastle
Bebe £7m Estrela - Man Utd
Thiago Silva £25m Milan - PSG
Radamel Falcao £45m Porto - Atletico Madrid
Jumla- £398.5 million
No comments:
Post a Comment