Kutoka Soccernet:
"Ikiwa vitu vitaendelea hivi, soka la Hispania litajiua lenyewe. Mwaka mmoja uliopita nilitabiri La Liga ina misimu 10 iliyobaki, sasa naona mitano zaidi itakuwa mingi sana.
Haki za matangazo ya TV ya La Liga zinauzwa vibaya kwa sababu kuna waendeshaji wawili wa matangazo hayo, wakati kwingine kote barani wanafanya mazungumzo kwa upande mmoja tu. Pia kwa maoni yangu nadhani Wachina wanapewa umuhimu usio na ulazima wakati Waamerika na Wajapan ndio wanaofaa kupewa kipaumbele.
Njia sahihi kwa vilabu vya Spain kuongeza mapato yao ni kuunda Iberian league, ambayo itahusisha vilabu vikubwa vitatu vya Ureno. Leo hii kuna katika msimu mzima kuna mechi chache sana zinazoweza kuvutia watazamaji. Kuongeza vilabu vitatu vikubwa vya Ureno kutaongeza msisimko - Porto, Benfica na Sporting Lisbon wataongeza ushindani na mvuto kwenye soka letu." Alimaliza Mchumi huyo.
No comments:
Post a Comment