Lakini katika jaribio la kupunguza uzito kama alivyoshauriwa na madaktari, mchezaji huyo bora wa wa dunia kwa mara tatu, ameamua kushiriki kwenye kipindi cha Television cha kushindana kupunguza uzito.
" Nina furaha kushiriki katika kipindi hiki kwa sababu ni muhimu sana kwangu kupunguza uzitoPia Ronny anasema anataka kufanikiwa kupunguza uzito ili aweze kushiriki kwenye mechi ya hisani pamoja na mchezaji mwenzie wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane mwezi wa 12 mwaka huu.
"Labda sikuwa na presha ya kila mtu kuniangalia nikijaribu kupunguza uzito ndio sikuweza kufanikiwa sana huko nyuma..
"Yote ninayowza kusema ni kwamba nitafanya sana mazoezi kwa juhudi mpaka nitaposhinda hii vita ya kupunguza uzito."
No comments:
Post a Comment