Search This Blog

Tuesday, September 4, 2012

MANCHESTER UNITED INAHITAJI KUFANYA MAREKEBISHO KWENYE SAFU YA ULINZI ILI KUURUDISHA UBINGWA KWENYE KABATI LA MAKOMBE OLD TRAFFORD

Okay, labda inaweza ikawa mapema kuanza kuwa na mashaka na ukuta wa timu ya Manchester United - hasa baada ya mechi ya jana iliyoisha kwa ushindi pale St Mary's dhidi ya Southmpton, lakini acha tuangalie uhalisia, Manchester United walionekana wadhaifu sana kwenye safu ya ulinzi.

Baada ya kuongezwa kikosi kwa Shinji Kagawa na Robin Van Persie katika safu ya ushambuliaji, mambo yanaonekana kuwa mazuri sana upande wa mbele na kutakuwa na magoli mengi ya kufunga msimu. Hilo limeanza kuonekana katika mechi 3 za mwanzo, Van Persie akiwa ameshatupia mabao manne katika mechi 3.

Pamoja na kukosa penati, van Persie aliweza kufunga hat-trick, mawili katika dakika za majeruhi na moja mwanzoni mwa mchezo, na kuisadia United kuondoka na pointi tatu.

Japokuwa, pamoja na kusubiriwa sana kurudi kwenye kikosi - mabeki wa kati wawili Rio Ferdinand na Nemanja Vidic - mambo bado yanaonekana kuwa mbali kurudi kwenye hali yake ya kawaida kwa vijana wa Fergie.

Misimu kadhaa iliyopita Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra waliunda ukuta wa hatari, kiasi cha kumfanya Edwin Van Der Sar acheze dakika 1,311 mfululizo bila kuruhusu wavu wake kuguswa. Kikosi chake hicho cha United kilimaliza msimu mzima kwa kuruhusu wavu wake kuguswa mara 24 tu.

Lakini sasa, zikiwa mechi tatu zimepigwa, United tayari imeruhusu mabao matano kwa timu ambazo kiuhalisia sizioni zikishandania nafasi za juu sana kwenye ligi msimu huu.

Mabao yote mawili ya Southmpton siku ya jumapili yalitokana na uzembe  wa mabeki kutoka mabeki wa pembeni, Rafael Da Silva na Evra. Katika mashambulizi yote ya magoli, mabeki hao walishindwa kiurahisi na washambuliaji wa Soton Rickie Lambert na Morgan Schneiderlin ambao walifumfunga kipa Anders Lingegaard.

Hata wale mabeki wanaochezaga vizuri Vidic na Ferdinand walionekana kucheza ovyo pia mbele ya washambuliaji wa Southmpton, ambao waliwafanya mapro wakubwa English Premier league kuonekana kama ndio wa kwanza wanagusa mpira kwenye ligi kuu.

Kiuhalisia - safu ya ulinzi ya United imeanza kuzeeka, hivyo kunahitajika kuwepo kwa warithi sahihi kuweza kuchukua nafasi ya wakongwe wa nafasi za nyuma.

Kurudi kwa Phil Jones kwenye beki ya kulia kutaondoa matatizo kadhaa kwa vijana wa Alex Fergie.

Rafael kama ilivyo kwa mabeki wengi wa kibrazil ni mzuri sana akiwa anaenda na mpira mbele kushambulia, lakini kumbuka jukumu lake kubwa ni kuzuia na sio kushambulia.

Jones ana ofa kwa usawa uwezo wa kushambulia na kuzia, pia mchezaji mpya Alexander Buttner aliyesajiliwa anaweza kuchukua nafasi ya beki wa kifaransa anayeonekana amechoka baada ya kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu -  Patrice Evra.

Buttner alikuwa akitegemewa kuwa mchezaji wa mbeleni, lakini kiwango kibovu kinachoonyeshwa na Evra hasa katika kuzuia katika shavu la kushoto la United kunamaanisha kwamba kinda hilo la kiholanzi litapigi lianza kupiga jaramba muda wowote Fergie atampa jukumu la kuulinda ukuta wa United upande wa kushoto.

Kuna matatizo kadhaa kwenye ukuta wa United ambayo yanatakiwa kutatuliwa katika siku kadhaa za hivi karibuni kabla hawajaendelea kupoteza pointi na timu ambazo hawastahili kupata pointi dhidi ya United. Van Persie na wenzie mbele sio siku zote hawatakuwa kwenye kiwango cha jana kuweza kuiokoa timu na aibu ya kufungwa.

Ikiwa United na Fergie wanataka kuurudisha ubingwa kwenye kabati la kuifadhia makombe pale Old Trafford basi lazima wafanyie marekebisho safu ya ulinzi ya timu hiyo.

No comments:

Post a Comment