Search This Blog

Tuesday, September 4, 2012

EXCLUSIVE: VODACOM KUIDHAMINI TENA LIGI KUU YA TANZANIA BARA KWA MIAKA 3

Hatimaye ligi kuu ya Tanzania bara imepata mdhamini, si mwingine ni yule yule mdhamini wa miaka kadhaa iliyopita kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.

Kwa taarifa za ndani na uhakika kabisa nilizozipata ni kwamba kamati ya ligi kuu inayoundwa na vilabu vishiriki vya ligi kuu imetiliana saini na Vodacom mkataba wa kuidhamini ligi kuu ya Tanzania bara kwa miaka mitatu kuanzia msimu huu.

Katika mkataba huo wa miaka mitatu vilabu vyote vya ligi kuu vitachukua zaidi ya millioni 65 kila msimu kwa ajili matumizi kadhaa, pia watapewa vifaa vyote vya kuchezea.

Pamoja na maboresho hayo kwenye mkataba mpya, pia suala la vilabu kuvaa jezi huku nembo ya mdhamini wa ligi kuu kuwepo kifuani limeondolewa kwa maana hiyo timu zitavaa jezi na kuweka nembo ya wadhamini wao binafsi wa timu husika kama ilivyo kwa ligi nyinginezo duniani - mfano mzuri England, Barclays ndio wadhamini wa ligi lakini Arsenal, Chelsea, Liverpool na vilabu vingine wanavaa jezi zenye nembo ya wadhamini wao binafsi.

No comments:

Post a Comment