Search This Blog

Tuesday, September 25, 2012

EDEN HAZARD AONGEZA CHUMVI KWENYE KIDONDA CHA TOTENHAM CHA KUKOSA NAFASI YA KUSHIRIKI CHAMPIONS LEAGUE

Msimu uliopita ulikuwa mzuri sana kwa Tottenham. Walimaliza katika nafasi ya nne na yalikuwa mafanikio mazuri tu, lakini japokuwa walimaliza nafasi mbili mbele ya Chelsea, watoto wa darajani waliweza kuleta huzuni White Hart Lane ambayo mpka leo inawaumiza Spurs.

Chelsea waliwafunga Spurs 5-1 kwenye nusu fainali ya FA Cup. Na kwa kushinda Champions League, Chelsea wakaipora nafasi ya Spurs ya kufuzu UCL, jambo lilopelekea Harry Redknapp kupoteza kazi na kurithiwa na Andre Villas Boas - mwalimu ambaye Chelsea walimfukuza na kumpa kazi Roberto Di Matteo mwalimu ambaye aliwapa mataji mawili Chelsea. Na sasa, Eden Hazard amezidi kupakaza chumvi kwenye kidonda cha Spurs kwa kwamba kitendo cha Chelsea kuwapora Spurs nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa wa ulaya pia kilimfanya asijiunge na timu hiyo ya London ya kaskazini.

Kutoka PA Sport:
"Ni kweli kwamba nilishawishika kujiunga nao kwa sababu ilikuwa ni timu ya vijana ambayo ilikuwa ikishika nafasi ya juu kwenye ligi,"  Hazard aliiambia France Football.
"Kwa bahati mbaya, mwishoni mwa msimu haukuwa mzuri. Hawakufanikiwa kuingia kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya, jambo ambalo linifanya niende upande mwingine.
"Ubingwa wa ulaya na kufuzu kucheza ligi ya mabingwa msimu huu, kulinifanya niichague klabu ambayo haikuwa imefanya vizuri sana kwenye ligi ya nyumbani. Pindi Chelsea waliposhinda ubingwa usiku ule Munich, tayari nilishapata jibu la wapi pa kwenda."

No comments:

Post a Comment