Renatus Njohole muasisi wa Njohole Foundation |
Wakati sekta ya michezo Tanzania ikiendelea kuzorota, baadhi ya wadau wa michezo wamekuwa wakitajitahidi kufanya wawezalo kuweza kuisadia michezo ipige hatua hapa nchini, lakini cha ajabu wamekuwa hawapati sapoti ya kutosha kutoka kwa serikali - hasa kupitia wizara yake ya michezo.
Baadhi ya wachezaji washiriki wa mechi hiyo ya uzinduzi wa Njohole Foundatio - Mwenye fulana ya njano ni Bakary Malima Jembe Ulaya |
Moja ya kitendo ambacho kimefanyika hivi karibuni, Taasisi ya Njohole Foundation ambayo ipo chini ya familia ya wacheza soka maarufu akina Renatus Njohole, Likembe Njohole na wengineo kwa ajili ya kuwasaidia wacheza soka wa zamani na wa sasa ili kuweza kuwa kuvitumia vizuri vipaji vyao katika kuiwezesha nchi kufanikiwa kimichezo na wao kunufaika vizuri na kazi yao ya soka.
Baadhi ya wachezaji watakaoshiriki katika mchezo wa mchezo wa kesho kati ya Njohole XI na mastaa wengine wa soka. |
Taasisi hiyo imeandaa mchezo maalum wa hisani ambao utawashirikisha wachezaji tofauti wa zamani na sasa katika kuizindua taasisi hiyo, na mapato yatakayopatikana yataingia katika mfuko wa foundation hiyo, ili kuweza kufanya vizuri shuguli hiyo taaisi hiyo ikapeleka maombi kwa Wizara ya Habari na Michezo kwa ajili ya kupewa ruhusa ya kutumia uwanja wa taifa kwa ajili ya kufanyika kwa mchezo huo, cha ajabu wakaambia ikiwa wanataka kuutumia uwanja huo itabidi walipe millioni 20.
"Tulikuwa tumetuma maombi ya kuweza kuutumia uwanja wa taifa kwa ajili ya mchezo huo, lakini serikali ikashindwa kuturuhusu mpaka tutoe millioni 20. Hili jambo limetushangaza sana kwanza wenyewe serikali ilibidi watusapoti kwa hali na mali katika kuweza kufanya mambo yetu, lakini badala yake wanataka tuwalipe millioni 20 ambazo zinaweza kusadia katika kuendesha shuguli za kila za foundation yetu, ikizingatiwa hatupati msaada wowote kutoka kwao."
Bakary Malima Jembe Ulaya akiwa mazoezini leaders Club |
Taasisi ya Njohole Foundation wanasema pamoja na kutoa mafunzo ya soka kwa vijana wadogo, pia itakuwa inachukua wachezaji wa zamani na kuwapeleka nje kusoma then watakapohitimu masomo yao watarudi nchini na kufundisha soka kwenye shule mbalimbali. Pia watakuwa wanatoa elimu kwa wachezaji namna ya kuweza kuzitumia vizuri fedha wanazopata katika soka ili kujiwekea misingi mizuri ya kimaisha mara pale watakapoacha kucheza mpira baada ya umri uwa mkubwa au sababu nyingine kama vile kupata majeraha yatakamfanya ashindwe kuendelea kuingia dimbani. ANGALIA VIDEO HIZI UONE WANA FAMILIA YA NJOHOLE WAKIONGELEA TAASISI YAO.
No comments:
Post a Comment