Search This Blog

Friday, August 10, 2012

JAMHURI KHWELU JULIO - SERIKALI HAINA MSAADA WA DHATI KWA WANASOKA WA TANZANIA

Baada ya serikali kupitia wizara ya Habari na michezo kukataa kuwapa uwanja wa taifa taasisi ya Njohole Foundation kwa ajili ya kucheza mechi ya uzinduzi wa taasisi hiyo, mmoja ya wachezaji wa zamani na kocha ambaye ameshazifundisha timu kadhaa ikiwemo timu ya taifa ya Tanzania under 17, Jamhuri Kihwelu Julio leo ametoa ya moyoni kuhusu wizara hiyo ya michezo na jinsi inavyofanya kazi zake katika kukuza na kuisadia michezo nchini.

Jamhuri Kihwelo anasema kwamba wizara ya michezo ya Tanzania haina msaada wowote na wanasoka wa sasa mpaka wa zamani waliowahi kulitumikia taifa hili.

"Wizara ya michezo haijali kwa dhati michezo ya Tanzania, wanafanya mambo kisiasa sana, na wanamuangusha Raissi Kikwete ambaye sio siri amejitahidi katika kusaidia michezo. Hawa watu wa Njohole wanataka kusaidia soka kwa kufundisha vijana na kupeleka makocha nje kusomea na kuja kufundisha kwenye shule lakini serikali inashindwa uwasapoti katika kuzindua shughuli zao, eti wanataka millioni 20 kwa ajili ya uwanja. Mbona TFF wanatumia uwanja huo na wanatumia mamilioni ya pesa lakini uwanja bado kila siku unaendelea kuwa na hali mbaya? Hizo millioni 20 zitwasaidia nini sasa. Hii ni kitu kufaidisha watanzania hivyo serikali ilibidi wasapoti kwa hali na mali.

"Hii tabia ya serikali kutaka fedha nyingi kwa ajili kutumia uwanja inaleta matatizo sana kwenye soka. Kwa mfano sasa hivi kuna hii michuano ya Super 8 ambayo imeshindikana kufanyika kwnye uwanja wa taifa kutokana na masuala hayo hayo serikali kutaka fedha nyingi kwa ajili ya mechi zinazochezwa hapo. Sasa hivi mivhuano hiyo inafanyika Chamzi, ambao ni uwanja mzuri lakini kwa wadhamini inakuwa tofauti kidogo, kwa kuwa wanakuwa hawapati nafasi nzuri ya kujitangaza, tofauti na mechi zinapofanyika kwenye eneo kubwa na zuri zaidi kama kwenye uwanja wa taifa. Hivyo pia kutokana na hivi hali hii itatukimbizia wadhamini ambao wamekuwa ni moja ya kilio cha muda mrefu kwenye michezo."

MSIKILIZE JULIO AKIWAPAKA WIZARA YA MICHEZO

No comments:

Post a Comment