NA EDO KUMWEMBE
Inaendelea kutoka wiki iliyopita.
NI swali linalowaumiza Watanzania wengi.
Je, Samatta anaweza kuuzwa kwenda kucheza Ulaya?
Watanzania wanatamani kumuona Samatta akiendeleza ndoto zake licha ya sasa kuwa staa wa TP Mazembe.
Wengi wangetamani kumuona akicheza moja kati ya ligi kubwa barani Ulaya, iwe Hispania, England, Ufaransa, Italia au Ujerumani.
Nikiwa na Samatta tukielekea katika sehemu moja ya chakula cha
mchana kinachopikwa na Watanzania inayoitwa Parachute, Samatta
anaonekana kuwa na hisia zile zile za Watanzania.
Bado nina kiu ya kucheza Ulaya.
Mimi hapa naona napita kwa sababu natamani sana kukipiga Ulaya.
Najua Watanzania wanachotaka na mimi bado sijabadili msimamo wangu, nikipata nafasi ya kucheza Ulaya tu namlilia Moise Katumbi.
Mtu mwenyewe anaonekana kuwa na huruma kidogo, anasema Samatta huku Thomas Ulimwengu akicheka.
Hili la Katumbi ndilo linaonekana kuwa kikwazo kikubwa katika
mazungumzo. Hata Samatta mwenyewe anakiri kwamba Katumbi ni tatizo kubwa
kwake kuuzwa Ulaya.
"Nimezungumza na Katumbi kuhusu mimi kucheza Ulaya lakini anaonekana hataki kabisa kusikia habari za mimi kuuzwa. Kuna wakati aliniambia wazi wazi kwamba timu inayonitaka lazima iilipe Mazembe kiasi cha Euro 10 milioni.
Mimi sina thamani hiyo na wala sidhani kuna mchezaji anayecheza Afrika ana thamani hiyo.
Nadhani hapo nia yake ni kutoniuza. Eti brother, haiwezekani timu itoe Euro 10 milioni kwa ajili yangu. Nadhani nikimwambia kuwa nataka kuhama lazima kutakuwa na kasheshe," anasema Samatta huku akicheka.
Hata hivyo, Samatta ananishangaza zaidi anaposema kuwa kuna ofa za kutoka Ulaya zimeshafika mezani kwa Katumbi kwa ajili yake.
Ananishangaza zaidi anaposema kuwa hata wababe wa Hispania, Real Madrid walishatuma maskauti wao wamtazame.
"Katumbi aliwahi kuniambia kuwa maskauti wa Real Madrid walisafiri
kuja kunitazama wakati tunacheza na Vita katika Ligi Kuu yetu hapa
Congo.
Ilikuwa mechi tuliyocheza Kinshasa, lakini siku ile mimi sikucheza
vizuri kwa hiyo sidhani kama walivutiwa au vipi,"
anasema Samatta.
Pamoja na hali hiyo, Samatta anakiri kwamba ili mchezaji wa Mazembe
atimize ndoto zake za kucheza Ulaya ni lazima akubali kuona kipato chake
cha pesa kinapungua, labda kama akisajiliwa na timu kubwa barani Ulaya.
"Hata hivyo, braza ukihama Mazembe kwenda Ulaya inabidi uende timu
inayoeleweka, kama ukienda timu ya kawaida pato lako litapungua sana kwa
sababu Mazembe inalipa posho nzuri kuliko hizo timu za Ulaya.
Unamuona huyu Kabangu (kiungo wa Mazembe aliyeuzwa kwenda
Anderlecht misimu miwili iliyopita) amerudi hapa na ameniambia amerudi
kwa sababu hapa wanalipa vizuri kuliko Anderlecht. Yupo hapa nadhani
unamuona ameshaongea na Katumbi na ameanza mazoezi.
Hapa tukishinda mechi kama hizi za kimataifa katika Ligi ya
Mabingwa, Katumbi anaweka dola laki tatu mezani (Sh 450 milioni).
Tunakuwa watu kama 25 na tunagawana pesa zote hizo.
Sasa kwanini tusiendeshe magari haya? Nadhani kuna klabu za Ulaya hazijafikia posho hizi.
Hata Katumbi mwenyewe amewahi kuniambia kuwa nikitoka hapa kama
naenda Ulaya inabidi niende kucheza timu kubwa iliyo juu ya Mazembe hata
kwa mapato."
Kwa fedha alizonazo Katumbi, ambaye pia ni Gavana wa Jimbo la
Katanga, huku mara zote akiwa anaonekana katika televisheni akifanya
shughuli mbalimbali za Serikali, namuuliza Samatta kama huwa anapata
muda wa kuzungumza na Katumbi.
"Huwa ananipigia simu mara nyingi. Lakini mpaka yeye awe na jambo
lake au ajisikie. Katumbi ana mambo mengi, mara utasikia yuko Ubelgiji
mara kesho asubuhi unamuona Lubumbashi.
Mimi nikimpigia simu haipokelewi, inaita tu. Halafu anaweza kunipigia hata saa nane usiku. Ni mtu mkubwa sana hapa."
Baada ya muda tunaenda Western Union ambapo Samatta anatuma pesa kwa baba yake nyumbani Tanzania. Ni kiasi kikubwa cha fedha, lakini huo unabakia kuwa utaratibu wake wa kila mwezi.
"Huwa natuma fedha nyumbani kila mwisho wa mwezi.
Ni kitu cha kawaida, Mzee Samatta lazima ajivunie kuwa na mwanaye au
vipi braza? Ndiyo maisha yalivyo, tunapata baraka za wazee.
"Hawa wachezaji wa Zambia kina Kalaba, Sunguluma, Sinkala ikifika
mwisho wa wiki wanaendesha magari yao kwenda hapo Ndola, si mbali ni
mwendo wa saa moja tu, mimi na Thomas (Ulimwengu) inabidi tutume fedha
tu nyumbani kwa sababu hatuna uwezo wa kurudi Tanzania mara kwa mara."
Asubuhi ya siku ambayo natakiwa kuondoka inafika. Lakini wote watatu, mimi, Samatta na Ulimwengu tunafunga mabegi.
Wao mabegi yao yanalazimika kusafiri kwa basi kwenda Ndola ambako
timu itaweka kambi, lakini wachezaji watasafiri jioni kwenda huko na
ndege yao binafsi.
Tunafika mpaka mazoezini kwa ajili ya kuwaacha na kisha nichukue
gari la Samatta kupelekwa uwanja wa ndege kuwahi ndege ya saa nne
asubuhi.
Tofauti na siku nyingine, safari hii hatupaki ile sehemu ambayo
Samatta huwa anapaki gari mazoezini. Hii ni kwa sababu Mfalme Mputu
anaweza kutuzuia na nikachelewa kwenda uwanja wa ndege.
Mnamwaribia Samatta hizi habari zenu zinasomwa mpaka Kinshasaa,mtamfanya dogoa akose ushirikiano kwa wenzake,hata huyo Mputu kama halikuwa hana wivu na dogo basi atakuwa nao,Jamani msidhani mnampaisha Samatta kumbe mnamwalibia,mimi kiupande wangu sidhani kama Mputu anaweza kumwonea wivu dogo kwanza kamzidi kila kitu kuanzia umaarufu mpaka kiwango cha kisoka,jamani hizo habari zunu kabla hmjazirusha ni better mkapata ushauri kwa watu wanaoweza kufikiri pande mbili...msiandike habari ilimradi mpate publicity pls stop writting this rubbish,it ll cost Samatta kama mnania naye nzuri kweli potezeeni hizo habari,hata Katumba atamwona dogo kama snitch.....
ReplyDeletefestchrist
Kweli kabisa unachofanya EDO co kumsaidia Samatha ila unamwaribia kama mwandishi wa juu alivyosema ni bora ukawa unapata ushauri kabla ya kukurupuka na kupost 2 vi2 online
ReplyDelete