Search This Blog

Tuesday, August 28, 2012

MTOTO WA MAFISANGO AILAANI SIMBA - AIMBIA ISIPOPELEKA RAMBIRAMBI HAITAFANIKIWA


 
MTOTO wa marehemu Patrick Mafisango anayeitwa Crespo (5) hataki kabisa kusikia habari ya kwenda Dar es Salaam.

Crespo ambaye kwa sasa anaishi nchini Rwanda aliiambia Mwanaspoti kuwa hataki kwenda Dar es Salaam kutokana na kutotaka kukumbuka kifo cha baba yake.

Kiungo huyo wa zamani wa Simba na Azam, Mafisango alifariki dunia Mei mwaka huu kwa ajali ya gari jijini Dar es Salaam.


Crespo ambaye, mama yake ni raia wa Rwanda, alikuwa akiishi na baba yake nchini Tanzania na hata alipofariki alikuwapo Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwanaspoti, Crespo alisema: "Kwenda Dar es Salaam hapana kwani sitaki kukumbuka mambo ya baba.

"Ninapotaka kwenda ni Congo tu kwa Mama Natalii (alikuwa mchumba wa Mafisango), tuchukue motoo (pikipiki) sasa hivi tufike Uwanja wa Ndege tuondoke lakini si kwenda Dar es Salaam," alisisitiza Crespo.

Mtoto huyo kwa sasa analelewa na bibi yake mzaa mama yake anayeitwa, Tatu Mwinyi katika mji wa Nyamirambo nchini Rwanda.

Yupo pia na ndugu yake Mafisango, Oly Lemba aliyepata ajali na Mafisango maeneo ya Chang'ombe Keko jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine, Oly ameelezea kwa masikitiko yake kufuatia kitendo cha Simba kugoma kutoa fedha za rambirambi za kifo cha Mafisango.

"Nasema kwa kitendo hicho, Simba haitakaa ifanikiwe pengine irekebishe suala la fedha za Mafisango na wasipofanya hivyo ipo siku watarudi kaburini walipomwacha," alisema Oly.

Simba imegoma kutoa fedha za rambirambi za kifo cha Mafisango zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa madai ilizitumia kulipia gharama za mazishi ya kiungo huyo.

Source: Mwanaspoti

No comments:

Post a Comment