Inapewa sifa kuliko inavyostahili? Labda. Lakini kuna sababu kwanini English Premier League inaonekana kwa upana zaidi kama ligi bora kabisa ya ndani ya nchi duniani kote.
Huku ikiwa na miaka 20 tangu kuanza kwake, Premier league imekuwa chombo kilichobadilishwa namna soka inavyoangaliwa, mpaka inavyochezwa.
Premier league ilizaliwa mwaka 1992 kutokana na matamanio ya vilabu vikubwa vya England kupata faida kubwa kutokana na haki za matangazo ya Televison.
Ulikuwa ni muda ambao soka la England lilikuwa linatoka kwenye muda ambao ulikuwa ni giza la uhuni, ukosefu wa mashabiki viwanjani na ukosefu wa mvuto.
Huku kukiwa na uwepo wa fedha nyingi, utangazwaji na hamu ya kutaka kuiteka dunia, Premier league inaendelea kuitawala tasnia ya soka duniani leo hii.
Hizi ndio sababu 5 kwanini Premier League ndio ligi bora duniani.
WINGI WA UPINZANI WA VILABU VYA NDANI
England ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na vilabu vya juu, ambavyo vinatoa utajiri wa wingi wa upinzani wa vilabu vya ndani.
Kuna kipute cha upinzani cha London ya kaskazini, kipute cha upinzani wa mji Birmigham na vipute vingine kibao vya ndani ya nchi hiyo....OK, kati ya mechi hizi hakuna inayoweza kuifikia utamu wa kipute kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona, au Boca Juniors dhidi ya River Plate - lakini kikubwa zaidi kuna mechi mbili tu kwa msimu zinazohusisha upinzani mkubwa, tofauti na England ambapo kila wiki kuna uwezekano wa kuangalia mechi ya upinzani wa juu.
MECHI KUTOKUTABIRIKA
Moja ya sababu kubwa nyingine inayoipa ubora ligi kuu ya England ni kutokutabirika kwa mechi.
Japokuwa ni ukweli kwamba ni vigumu kwa timu kama Southmpton kuwa mabingwa bila msaada wa matajiri wenye za kutupa kama akina Shekhe Mansour , lakini premier league bado inatoa level ya juu ya suhindani kutofautisha na ligi nyingine duniani.
Imekuwa kitu cha kawaida sana kuona Manchester United ikifungwa na timu ndogo au ikipata shida sana kupata japo sare. Tofauti na Spain ambapo inapocheza Barelona na Recreativo Huelva unajua leo Lionel Messi anatupia hat trick ngapi, lakini ni vigumu kufikiri hivyo inapocheza Chelsea na Reading au Manchester City na QPR.
Ikumbukwe moja ya mechi zilizosababisha Manchester United kukosa ubingwa kwenye dakika za mwisho ilikuwa dhidi ya timu iliyokuwa ikipambana kushuka daraja Wigan, - Ni vigumu kuona Real Madrid wanafungwa na timu inayoshika mkia kwenye la liga.
UPINZANI WA VILABU VIKUBWA
Mbali wa upinzani mkubwa timu zinazotoka sehemu moja: mfano Aston Villa vs Birmigham. Pia kuna wingi wa upinzani wa vilabu vikubwa.
England kuna utamu wa Mechi mbili za Manchester United dhidi ya Man City, Liverpool vs United, Arsenal vs Chelsea, Tottenham vs United, Arsenal vs Tottenham, United vs Chelsea,Tottenham vs City, Arsenal vs United, City vs ARsenal na nyingine kibao.
Mechi za namna hii ni vigumu kupata kwenye ligi nyinginezo duniani.
USHINDANI
Moja ya hoja wanazotoa wapinzani wa Premier league ni ukosefu wa ushindani, hoja ambayo inakuja kutokana na ligi kuu ya England tangu uanzishwa kwake Manchester United imechukua ubingwa mara 12 kati ya 20.
Lakini hao hao United wamekuwa sio watawala wa ligi kuu ya England wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye mashindano ya kimataifa. Katika cha miaka mitano iliopita United wamecheza fainali 3 za champions league. Hii inaonyesha ni kiasi gani England inatoa bingwa sahihi.
Premier league pia imekuwa ikitoa nyingi kwenye mashindano ya kimataifa ambazo zimekuwa zikifanya vizuri.
Mwaka jana Manchester City ilikuwa ni klabu ya tano kushinda ubingwa wa EPL. Mabingwa watano tofauti kwenye kipindi cha miaka 20. Huu ni uwiano mzuri wa ushindani. Sasa Angalia ligi ya Spain, kwenye kipindi cha miaka 20 iliyopita imetoa mabingwa wanne, huku katika katika historia ya ligi hiyo tangu kuanzishwa kwake miaka 90 iliyopita imetoa mabingwa tisa tu.
MAFANIKIO YA ULAYA
Moja ya sababu kubwa ya kufanya mapinduzi ya kuileta Premier League ilikuwa ni kuleta upinzani mkubwa ambao ungetosha kuwafanya kuitawala soka la bara la ulaya.
Ilichukua miaka kadhaa, lakini kwa sasa inaonekana wamefanikiwa vizuri sana.
Makombe manne kati ya 20 ya champions league yamechukuliwa na vilabu vya Premier League, matatu kati ya hayo ndani ya miaka 10 iliyopita. Fainali tano za champions league zilizopita zimekuwa zikihusisha vilabu vya England - United na Chelsea.
Kama, wengi wanavyosema kwamba Champions league ndio roho ya ubora wa soka, basi Premier league inastahili kuitwa ligi bora duniani.
By Aidan Seif Charlie
No comments:
Post a Comment