Search This Blog
Monday, August 27, 2012
MOSHI WAPATA UONGOZI MPYA KWENYE SOKA
Na Dixon Busagaga ,Moshi
CHAMA cha soka cha manispaa ya Moshi(MMFA) na kile cha wilaya ya Hai (HFA) vimepata viongozi wapya watakao viongoza kwa kipindi cha miaka minne ijayo huku sura mpya za vijana zikitawala zaidi katika nafasi mbalilmbali za juu.
Katika chaguzi hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki,Japhet Mpande alichaguliwa kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama cha soka manispaa ya Moshi huku nafasi ya mwenyekiti ikichukuliwa na Godfrey Madegwa.
Mchezaji wa timu ya Moshi veteran Tumain Mungete alichaguliwa kushika nafasi ya katibu mkuu wa timu hiyo na msaidizi wake ni alichaguliwa Laurance Munyonyi huku nafasi ya mweka hazina wa chama hicho akichaguliwa Thabiti Abdalah.
Nafasi ya mwakilishi wa vilabu alichaguliwa aliyewahi kuwa katibu msaidizi wa chama hicho Amri kiula huku wajumbe wakichaguliwa Abdalah Mtwenge,Shadrack Lema na Idd Nyangasa ambao wote walichaguliwa kutokana kuwa ndio wagombea pekee.
Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Nurdin Hussein amesema viongozi hao wote walichaguliwa kwa kupigiwa kura licha ya kwamba ndio walikuwa wagombea pekee katika nfasi hizo.
Alisema ushindani ulikuwa katika nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu ambapo aliyekuwa makamu mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro Darabu Maulid Darabu alijitosa kuwania nafasi hiyo akishindana na Goodluck Mushi.
Hata hivyo nafasi hiyo ilichukuliwa na Mushi baada ya kumbwaga Darabu maarufu kama Born Leader kwa kura 24 kwa 21 huku kura sita zikiharibika .
Katika uchaguzi wa chama cha soka wilaya ya Hai, Haroid Kifunda
alichaguliwa kushika nafasi hiyo baada ya kupata kura 19 akimshinda mpinzania wake Shabani Lema aliyepata kura 15 huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikiachwa wazi kutokana na wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kutokuwa na vigezo.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wilayani humo Martha Mathayo alimtangaza Cuthbert Mushi kushika nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho baada ya kuwa mgombea pekee aliyejitokeza huku nafasi ya katibu msaidizi akichaguliwa Awia Kimaro baada ya kuwa mgombea pekee pia.
Mjumbe wa mkutano mkuu alichaguliwa Haji Husant huku Wilbad Ngaro akichaguliwa kushika nafasi ya mwakilishi wa vilabu na nafasi zawajumbe kubaki wazi kutokana na kukosekana kwa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment