Luka Modric akipimwa vipimo vya afya katika hosptiali ya Real Madrid |
Tushukuru mungu, saga la usajili wa Luka Modric lilodumu kwa takribani miaka miwili sasa linaelekea kumalizika hivi karibuni baada ya Real Madrid na Tottenham Hotspur kukubaliana ada ya uhamisho na Modric anategemewa kusaini mkataba wa miaka 5 atakapofaulu vipimo.
Kwa bahati mbaya, Real Madrid hawakuweza kujizuia furaha yao siku mbili kabla. Wakiwa ndio timu pekee iliyokuwa ikimfukuzia Modric, Magiant hao wa kihispania wakaweka tangazo kwenye website yao kuhusu Modric kabla ya dili halijakamilika, na ikabidi walitoe masaa kadhaa baadae.
Bahati nzuri kwa Madrid hawapo peke yao katika vilabu ambavyo vimewahi kutangaza usajili wa achezaji kabla haujakamilika rasmi.
DAVID BECKHAM KWENDA BARCELONA
Sasa hivi kila mtu afadhali anajua kwamba Sir Alex Ferguson na David Beckham walishagombana kabla ya uhamisho wake kwenda Real Madrid - lakini sio watu wengi wanajua kwamba Manchester United walitangaza kwamba alikuwa akielekea kujiunga na Barcelona muda mchache kabla ya uhamisho wake wa kwenda Bernabeu.
"Naweza kutangaza kwamba tumekubaliana bei ya uhamisho na Manchester United kumnunua David Beckham," alisemamgombea uraisi wa Barca Joan Laporta, huku akipata sapoti kutoka kwenye taarifa ya United
Katika jaribio la kutaka labda kuwapa presha Madrid kutoa ofa nzuri au kukosoa bahati mbaya, lakini mwisho wa siku mhariri wa mtandao wa United alipoteza kazi yake.
JOHN OBI MIKEL KWENDA MANCHESTER UNITED
Ulikuwa ni uhamisho ulioleta utata mkubwa hapo nyuma, kinda lililokuwa likionyesha kila aina ya ishara ya kuja kuwa moja ya kiungo bora duniani - John Mikel Obi alikuwa akitakiwa na Chelsea na Manchester United.
Obi ambaye kipindi hicho alikuwa akiichezea klabu ya Lyn-Oslo akachagua kujiunga na Manchester United, na akaenda kutambulishwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari akiwa amevaa jezi ya United ikiwa na jina lake Mikel na namba 21 - jambo ambalo liliashilia mwisho wa saga hilo la usajili.
Baadae Mikel akatangaza matamanio yake ya kutaka kujiunga na Chelsea huku klabu hiyo ya London ya magharibi ikitangaza imekuabliana ada ya uhamisho mwaka mmoja uliopita. Ukatokea mtafaruku mkubwa kati vilabu vitatu, lakini mwisho wa siku Chelsea ikalipa £16 million na Oslo na United zikagawana pasu kwa pasu.
ROBINHO KWENDA CHELSEA
Chelsea wakapewa ladha ya dawa yao wenyewe mwaka 2008 baada ya kuanza kutangaza mauzo ya jezi yenye jina la Robinho, ambaye baadae akaamua kujiunga na Manchester City.
The Blues walijiamini kwamba wameshinda vita ya kuwania saini ya Robinho kiasi cha kufikia kuweka rasmi jezi ya Robinho sokoni, maskini ya mungu wale walionunua mpaka leo wanasubiri dili kutangazwa rasmi na mchezaji waliyenunua jezi yake atapewa namba ngapi.
RONALDO KWENDA FLAMENGO
Huko nyuma mwaka 2009 Ronaldo akaamua kurudi nyumbani Brazili kumalizia soka lake na klabu ya Flamengo. Alifanya nao mazoezi, raisi wa klabu akatangaza dili linakaribia kukamilika na Ronaldo mwenyewe akathibitisha anataka kujiunga na klabu yake ya utotoni. Lakini kwa bahati mbaya haikutokea kama ilivyopangwa, De Lima akajiunga na mahasimu wa Flamengo - Corinthians.
Jezi zikachomwa na mashabiki walikasirika sana LAKINI Ronaldo akasepa Flamengo.
MBUYI TWITE KWENDA SIMBA
Sakata la mchezaji limeleta kizazaa kikubwa sana kwenye soko la uhamisho nchini Tanzania.
Simba baada ya kuporwa mchezaji wao Kelvin Yondani aliyetimkia Yanga, wakacheza Kagame wakiwa na mabeki vimeo na wakatolewa kwenye robo fainali na Azam, japokuwa hawakupata chochote kwenye Kagame Cup lakini walibahatika kuona beki ambaye angefaa kuziba pengo la Kelvin Yondan, mchezaji wa APR ya Rwanda Mbuyi Twite.
Kagame Cup ilipoisha, Mwenyekiti wa Simba akapanda pipa mpaka Kigalia na akafanikiwa kumzidi mbio Bin Kleb wa Yanga ambaye alikuwa nae akimvizia Twite, ambaye akasaini mkataba wa kuicheza Simba na akapiga picha Rage - kisha ksiku kadhaa baadae kwenye tamsha la Simba day akapewa jezi namba nne. Simba wakaona vita imeisha - kumbe walijidanganya.
Yanga kupitia Bin Kleb wakarudi tena Kigali na wakafanya umafia mwingine na kufanikiwa kumshawishi Mbuyi Twite kujiunga na klabu yao na arudishe fedha za Simba. Kupitia vifungu vya sheria ambavyo inasemekana Simba walishindwa kuvitimiza kwa kusudi au bahati mbaya - Yanga wamefanikiwa kumtwaa Twite na tayari ameshaanza kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani kwenye mechi za kirafiki huku Simba wakisema wana RB yake akifika tu Dar wanamkamata.
Vita bado inaendelea hiiii
By Aidan Seif Charlie
No comments:
Post a Comment