Manager wa Manchester United Sir Alex Ferguson amewakataza wachezaji wenye umri wa klabu hiyo kuendesha magari ya kifahari kutoka kwa mdhamini wao mpya Chevrolet.
United hivi karibuni walisaini mkataba wa mamilioni ya paundi na kampuni hiyo kubwa ya kutengeneza magari kutoka Marekani, na watakuwa wadhamini wao rasmi wa jezi kuanzia msimu wa 2014-15.
Kama kuonyesha ishara ya urafiki mzuri mpya wa kibiashara baina yao na United, Chevrolet kwa haraka walitoa ofa kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha United kuchagua magari ya kifahari wayatakayo na wangepewa bure na vijana wengi wakaagiza magari aina ya Iconic Corvettes.
Marufuku kwa wachezaji wachanga wa Fergie |
Ingawa inasemekana Ferguson akaingilia kati na kuweka sheria kwamba vijana wa chini ya miaka 23 - haijalishi wana ukubwa na umuhimu gani kwenye timu - hawatoruhusiwa kutoa oda ya aina hiyo ya gari la kifahari.
Kwa maana hiyo wachezaji kama Danny Welbeck, 21, Phili Jones 20, Chris Smalling 22, na Rafael 22, na wengine kibao hawatoruhusiwa kuendesha magari ya kifahari ya ofa kutoka Chevrolet aambayo yatakuwa hayajapata baraka kutoka kwa Mzee Fergie.
Uamuzi huu wa Ferguson unalenga kuhakikisha vijana wake wadogo hawavimbi vichwa na kujisahau isivyostahili. Pia hii sio mara ya kwanza kwa Fergie kufanya kitendo kama hiki, miaka miwili iliyopita alitoa katazo kwa vijana wa timu ya watoto kutovaa viatu vya bei mbaya hasa vya rangi.
1. "Awakataza kutoendesha" maana yake ni kwamba amewalazimisha waendeshe magari ya kifahari
ReplyDelete2. "Alitoa katazo kutovaa viatu" maana yake ni kwamba aliwalazimisha wavae viatu vya bei mbaya
Lugha si ngumu, ila inategemea upeo na uelewa wa mwandishi!
Kaka Shaffih, mimi ni mmoja wa wadau wazuri wa blogu yako, ili kupata habari za michezo hususani za ndani kwakuwa siko TZ. Hata hivyo, sifurahii jambo moja. Hauko makini na matumizi ya lugha. Unaandika makosa mengi sana ya lugha. Hii ni blogu kubwa sasa na ndiyo maana una wadhamini. Tafuta mtaalamu wa lugha awe anakusaidia kuhariri habari zako. Hii itaongeza thamani ya blogu yako. Katika habari hii "Kali ya leo: Ferguson awakataza wachezaji chini ya umri wa miaka 23 wa United KUTOENDESHA magari ya kifahari" maana yake Ferguson amewaruhusu.
ReplyDeleteKanuni ya lugha, hata Kiingereza, ukikanusha maradufu unakuwa umeyakinisha (double negative=affirmative). Hapa ulipaswa useme tu: "Kali ya leo: Ferguson awakataza wachezaji chini ya umri wa miaka 23 wa United kuendesha magari ya kifahari".
Najua kuwa hili ni moja ya makosa mengi yanayofanywa na wanahabari wetu hapo TZ. Wewe unapaswa kuwa kioo kwakuwa ni kijana na una fursa nzuri ya kujifunza zaidi ili kujitofautisha na wao. Ni mchango wangu tu kwa lengo la kuboresha kazi nzuri unayofanya.