Makamu wa Raisi wa AC Milan Adriano Galliani amemwagia maji ya baridi kwenye mvuke wa tetesi zilizokuwa zikisambaa kwamba klabu hiyo ipo njiani kumsaini kwa mara nyingine Ricardo Kaka kutoka Real Madrid kutokana na matatizo ya kifedha.
Rossoneri wamekuwa kwa muda mrefu wakitafuta kusajili mchezaji mkubwa kwenye kipindi hiki cha kiangazi ili kuweza kupoza hasira za mashabiki waliodhiwa na kitendo cha kuuzwa kwa Thiago Silva na Zlatan Ibrahimovic kwenda PSG, lakini jitihada za mabosi wa AC Milan wamekwama kumsajili Mbrazil Kaka kutokana na kodi.
"Kodi ndio tatizo kweli kabisa. Ni kubwa sana. Tumejaribu kupata maoni ya kiuchumi kutoka makarani wetu wa fedha na wakatuambia utakuwa usajili wa gharama ambao hauendani na hali ya kifedha klabuni" - alimaliza Galliani
No comments:
Post a Comment