Search This Blog

Monday, August 6, 2012

EXCLUSIVE: SIMBA YAMSAJILI REDONDO KWA MILLIONI 30- ASAINI MKATABA WA MIAKA 2

Klabu ya Simba imeendelea kufungua makucha yake katika soko la usajili, baada ya wiki iliyopita kumtwaa Mbuyi Twite na Mrisho Ngassa, leo hii klabu hiyo imefanikiwa kumsajili kiungo wake wa zamani aliyekuwa akiichezea Azam Ramadhan Chombo Redondo.

Kwa taarifa rasmi nilizozipata kutoka kwa Redondo mwenyewe ni kweli amesaini mkataba na Simba akitokea Azam baada ya mkataba wake kumalizika. "Nimesaini mkataba wa miaka miwili na Simba nikiwa mchezaji huru baada ya mkataba wangu na mwajiri wangu wa zamani  Azam kumalizika"

Redondo ambaye aliondoka Simba takribani miaka 3 iliyopita, amesaini Simba kwa ada ya millioni 30, leo pekee wakati akisaini amepewa shilingi millioni 20, na millioni 10 zilizobaki atamaliziwa baadae.

10 comments:

  1. Karibu nyumbani chombo. Sasa tunataka okwi arudi kundini. Dawa ya yeboyebo ni tano tu.

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli bado tunahitaji kiungo?

    ReplyDelete
  3. Napata hofu kua ni kweli usajiri unaofanyika ni kocha anahusika au kutokana na mapenzi ya hao wenye influence katika kufanya huo usajiri...sijakubaliana na huo sababu simba hawakuhitaji watu kwenye nafasi hiyo sababu kuna namba ambazo kama wamezifumbia macho mfano hakuna msaidizi wa Sunzu na kutoona kua hajawa msaada katika timu na ndoma leo okwi kawa kama malaika kwetu...tuangalie wadau na viungo wote wale pia wanaongeza wengine!!karibu redondo ufanye kazi maana ndo ushasajiriwa na kua mchezaji halali wa simba.

    ReplyDelete
  4. naomba viongozi wangu wa simba waongeze nguvu kule mbele na beki pia Redondo karibu

    ReplyDelete
  5. Redondo ni muhm sana sunza atasaidiana na ngasa akitokea pemben huku mtukutu boban akisambaza na huku kiungo akicheza mbiyavanga akisaidiana na redondo au mude sasa angalia beki hyo mbuyu twinte na jembe kapombe na tyaison .tutaonana ligi kuu

    ReplyDelete
  6. Kuna mtu anakuja kutoka ivory coast nafikiri kuna kiungo mgeni itabidi aondoke na ndo mana chombo karudi. Usikonde kaka kikosi kitatulia tu.

    ReplyDelete
  7. da simba hyo nguvu ya soda mie nadhani mnaweweseka kwa yanga kuchukua kagame yan mnakurupuka ka arsenal

    ReplyDelete
  8. we chizi nini? mbona wote hao mliwataka mkawakosa au na nyie bado mnaweweseka na zile tano? tupisheni yeboyebo mambo ya mnyama hayawahusu. mbona hamuwezi kukaa kimya?

    ReplyDelete
  9. YAANI KILA TUNALOFANYA LINAWAUMA HAWA YEBO, HAWAWEZI HATA SIKU MOJA KUKAA WAKAANGALIA NA KUSHUGHULIKA NA YAO. YAANAI KABLA HAWAJAITWA WANAITIKA SIJUI WAKOJE MASKINI. MANJI ANAWADANGANYA KAMSAJILI OKWI BASI WAO WANAMUAMINI, NGOJENI TU MTAMTOLEA ROHO MBAVUNI HUYO GALASA WENU. NYIE KUPATA KAGAME MMEMALIZA LIWEKENI KABATINI MSUBIRI LIGI NA BWANA ILTON CAMEROON KAOMBA KAZI KENYA NA AMEFANIKIWA.KISHA KMAE KIMYAA CHUMBANI SIYE WACHEZAJI WANAJIANDAA NA CAF, BADALA MUWAZE 2014 ITAFIKA LINI MNAIANGALIA SIMBA HAYA!

    ReplyDelete