Mwalimu wa zamani wa shule na polisi mstaafu waliniambia namna ya mshambuliaji wa kati anavyopaswa kukaa ndani ya uwanja. Nilikuwa nafanya kozi yangu ya ukocha chini ya beji ya UEFA na huku nikiwa sitaki kuwakosea heshima walimu wale wawili, walikuwa wananichekesha kwa ushauri wao. Lakini pia kubwa zaidi niligundua uzito wa matatizo yanayolikumbuka soka la kiingereza. Najua namna ya kucheza kama mshambuliaji wa kati. Nimecheza kama mshambuliaji wa kati kwa miaka 20, tena zaidi kwenye level ya juu. Kama Maradona au Van Basten wangekuwa wananifundisha, ingekuwa sawa, lakini sio mwalimu mstaafu au polisi.
Mabadiliko yanatakiwa kufanyika katika hatua zote ili kuiwezesha England kuimarika na kuwa bora. Watu wanaondesha soka hawajawahi hata kucheza mchezo wenyewe, watu wanafundisha soka wakiwa hawajawahi au wamecheza kwenye level ya chini sana. Kuna watu kwenye soka la Uingereza wanapata kazi fulani kwa sababu wana urafiki au undugu na watu ambao tayari wapo kwenye system.
Sio kwamba wana makocha wengi. Pamoja na uwa wachezaji wachache waliosajiliwa, Spain wana makocha walio bora mara 10 kuliko sisi, wengi wao wakiwa wachezaji wa zamani. Walijenga msingi mzuri na sasa wanakula matunda..
Ndio maana nasisitiza hatupaswi kuwalaumu wachezaji wa England kwa kutofanya vizuri. Wanafanya kile ambacho walifundishwa. Tusiwalaumu kwa makosa na mbinu za kufundishia zilizopitwa na wakati za England.
Mabadiliko pekee kwenye Euro 2012 ni kwamba England walienda kwenye michuano huku wakiwa na mategemeo madogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya historia ya kutofanya vizuri kwa miaka kadhaa mpaka pale tulipoongoza kundi bila kutegemea. Taifa likaanza kujipa moyo na kuanza kuwa na mategemeo makubwa na wengine wakaanza kuamini England itaifunga Italy. Sikumbuki hata kama Buffon aliokoa japo mara mbili mashambulizi ya hatari katika dakika 120.
Roy Hodgson alifanya kama alivyotegemewa. Aliifanya England kuwa ngumu nyuma - lakini kwa gharama ya kukosa mashambulizi . England ilirudi miaka 10 nyuma na washambuliaji kama Rooney walipata taabu na kikosi kilichoundwa kulinda zaidi.
England haina wachezaji wengi aina ya Paul Scholes, ambao wapo comfortable na mpira. mashabiki hawasaidii pia. Wanategemea kuona damu ikimwagika ushindi upatikane, wachezaji kucheza kwa miguvu na kucheza kwa vyovyote vile ili mradi mpira uende mbele. Soka limebadilika - timu bora duniani sasa inacheza bila kuwa na mshambuliaji wa kati, wakati England bado inacheza kwa mipira mirefu na kutegemea krosi.
Wakati Ujerumani iliporudiwa mchezo kama huo dhidi ya Italy katika nusu fainali, waitaliano kwa urahisi waliifunga Ujerumani.
Mfumo wa soka la kiingereza inabidi kubadilika. Hakuna namna anaweza kutokea Xavi au Iniesta kwa mfumo huu wa kiingereza kwenye soka kwa sababu wataambiwa ni wadogo sana kwa maumbo yao. Kwa soka la kiingereza kilicho kuwa kikitakiwa ni kuwa kasi na nguvu basi - mpaka Barcelona walipoizima hiyo nadharia hiyo. Shukrani kwa Sir Alex Ferguson aliweza kumruhusu mtu mwenye umbo dogo asiye na kasi wala nguvu sana kama Paul Scholes kucheza.
Nchini England, watu wanauliza "Je anaweza kuzunguka uwanja wote?" wanaangalia namna mchezaji anayoweza kukimbia na kuzunguka uwanja akiwa anasaka mpira, wanaulizia namna mchezaji anayoweza kuweka mguu wake popote ili mradi kuhakikisha timu yake inapata matokeo. Waingereza tumeng'ang'ania kuangalia udhaifu kuliko uimara. Je Andrea Pirlo anazunguka uwanja mzima akisaka mpira kwa nguvu na kasi? Hapana. Kama ilivyo kwa viungo bora, anajipanga vizuri, anazuia, na ana intercepts na kugawanya mipira vizuri kwa wachezaji wenzie. Hahitaji kukimbia sana na kuingia kwenye miguu ya watu, au kutumia nguvu sana kukaba. Anachofanya zaidi ni kuji-position vizuri kuliko kutengeneza contact na wapinzani, soka la kiingereza sasa limekuwa kama NBA.
Timu sasa zinajua zinaweza kuidhuru England kwa kukaa na mpira tu. Niliwahi kuangalia michuano ya vikosi vya wachezaji nane nane nchini Hispania hivi karibuni ambayo pia iliwashirikisha wachezaji wenye umri wa miaka 15 kutoka kwenye vilabu vikubwa. Pia nimekuwa nikiangalia sana mpira wa vijana na nimemshuhudia mwanangu wa kiume Devante akicheza soka akitokea kwenye shule za soka za kiingereza kama mie. Level ya ufundi ya watoto wa kihispaniola ilikuwa kubwa sana kufananisha na England. Kucheza kwenye uwanja mdogo kunasaidia kwa sababu wachezaji wanagusa mpira mara kwa mara. Unaweza kuugusa mpira mara 15 kama straika katika mechi inahusisha wachezaji 11x2. Utapata mipira mingi zaidi katika mechi inayohusisha wachezaji nane na nane, lakini Wingereza wamekuwa wakiendekeza kuwafundisha wacheza wachanga kwa mechi za wachezaji 22 dimbani.
Sasa nini kinafuata kwa England? Ningekuwa mie ningewapa makinda nafasi; wachezaji ambao wamefundishwa kwenye level ya klabu kama Welbeck, Wilshare, Cleverley, Rodwell....
Fanya kila kitu ambacho wajerumani walifanya katika kubadilisha, then fikiria nini kitatokea katika miaka miwili, na sio miezi miwili. Kwa huzuni natamka, nina wasiwasi hakuna kitakachobadilika. Hilo linatokana na historia na sifa ya soka la Uingereza.
No comments:
Post a Comment