Kwa mujibu wa tovuti ya Azam Fc Mchezaji John Bocco amerejea kwenye kikosi cha Azam FC baada ya majaribio ya wiki mbili.
Maribio hayo yaliishia kwa kukubalika na kocha mkuu wa Super Sport United Gavin Hunt lakini bahati mbaya uongozi wa SUFC ulishindwa kutoa ofa ya kueleweka kwa John Bocco na Azam FC.
SuperSport United FC ilimtaka Bocco kwa mkopo huku wakisema kuwa kwa sasa hana uwezo wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu yao.
Lakini pia SUFC ilishindwa kuweka wazi maslahi ya mchezaji. Maelezo ya Uongozi wa SuperSport United FC ilikuwa ni kumuomba Bocco kwa mkopo kwa kuwa wanahitaji kumuona kwanza akifunga kwenye ligi ya Afrika ya Kusini kabla hawajafikiria ofa ya kumnunua.
Wakala wa mchezaji John Bocco Bw. Yusuf Bakhresa aliwataka Supersport United kumuonesha mkataba ambao wataingia na John Bocco na kueleza maslahi ambayo watakuwa wakimlipa lakini ilishindikana zaidi ya kusisitiza kuwa wanahitaji muda kabla hawajaingia mkataba mzuri na Bocco.
Yusuf hakufurahishwa na kitendo hicho na aliwataka SUFC kuwa wawazi kama wanamtaka John Bocco na watoe ofa itakayoizidi Azam FC vinginevyo itakuwa vigumu kumpata.
Azam FC imeamua kubaki na nyota wake huyu mwenye umri wa miaka 23 lakini milango ipo wazi kwa SuperSport kuendelea kumfuatilia na itakapotokea kuwa wamejiridhisha na kiwango chake basi walete ofa yao.
John Bocco binafsi baada ya kurejea nchini alisema amefurahishwa na mazingira ya Supersport United lakini akaomba kuwa angependa kupata maslahi makubwa zaidi ya Azam FC vinginevyo haoni sababu ya kwenda Afrika ya Kusini bila maslahi mazuri kwani Azam FC sasa ni timu kubwa Afrika Mashariki na mwakani itashiriki mashindano ya shirikisho barani Afrika.
No comments:
Post a Comment