Search This Blog
Tuesday, July 10, 2012
PAOLO HENRIQUE GANSO ASEMA ANAONDOKA SAO PAOLO - ANGALIA MAVITU YAKE UJUE KWANINI ATAIBUA VITA NZITO KWA VILABU VYA ULAYA
Paulo Henrique Ganso amecheza mechi yake ya mwisho akiwa na Santos, kwa mujibu wa mwakilishi wa mchezaji Delcir Sonda, lakini mazungumzo ya kuhamia premier league yanaonekana bado machanga, atleast kwa muda huu.
Ganso amekuwa na mgogoro na Sao Paolo juu ya mkataba mpya na kiungo huyo mwenye miaka 22 amekataa ofa mpya ya klabu hiyo.
"Hii ni sahihi kabisa, Ganso hatoichezea tena Santos. Na ndio anaweza kujiunga na klabu ya Internacional," Sonda aliambia Radio Estadao ESPN. "Nipo kwenye majadiliano na Santos kununua haki zake zote."
"Ganso amekasirishwa na klabu. Wameweka mpango kabambe kwa ajili ya Neymar na kumsahau Ganso. Anataka kuondoka lakini amesema anataka kubaki Brazil japo kwa mwaka mmoja zaidi."
Habari hizi zitaibua vita kubwa kutoka kwa vilabu vya ulaya, lakini Santos bado hawajakata tamaa kumrudisha klabuni hapo baada ya Olympics.
Santos manager Muricy Ramalho aliambia Lancenet: "Hatupo tayari kumpoteza Ganso, lakini tayari ameshaamua wapi anataka kucheza. Tunataka aondoke akiwa kwenye kiwango kizuri kwa ajili ya Olympics na baadae ikiwezekana arudi tena kwetu."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment