Search This Blog

Tuesday, July 10, 2012

BAADA YA RIQUELME KUTANGAZA KUHAMA BOCA JUNIORS - MASHABIKI WA TIMU HIYO WAANDAMANA NCHI NZIMA KUPINGA



Muda mfupi baada ya Boca Juniors kufungwa na Corinthians kwenye fainali ya Copa Libertadores, kiungo wa miaka 34, Juan Roman Riquelme alitangaza nia yake ya kuondoka kwenye klabu hiyo kwa mara ya pili. Ilikuwa habari mbaya sana kwa mashabiki wa Boca Juniors ambao walipata taarifa kwamba shujaa wao anapanda ndege ndege kuelekea Brazil kujiunga na Flamengo.
Hivyo huku Riquelme akijiandaa kuondoka, kama alivyofanya mwaka 2002 alipojiunga na Barcelona, maelfu ya mashabiki wa Boca waliungana mitaani kuandamana kwenye miji tofauti nchini Argentina kumuomba Riquelme asiondoke.Mkusanyiko mkubwa zaidi uliwahusisha mashabiki takribani 5000 pale La Bombonera mjini Buenos Aires, ambapo mashabiki hao walikusanyana mitaani mpaka kwenye uwanja huo. Kwa mujibu wa Ole, klabu hiyo mwanzoni walisema hawatowaruhusu kuingia uwanjani kwa kuwa hakukuwa na ulinzi, lakini baadae waliwaachia washabiki kuingia uwanjani huku wakiwa mabango ya kumuomba mchezaji wao kipenzi asiondoke huku wangine wakiimba "Riquelme ni Boca, Boca haondoki!"

Jambo kama hili lilishawahi kutokea jijni London wakati Manuel Almunia alipoondoka Arsenal.

Kwa ujumla, Riquelme amekaa miaka 12 na Boca Juniors, akicheza mechi zaidi ya 300, akishinda makombe matano ya Primera Division na makombe matatu ya Copa Libertadores. Alikuwa mchezaji bora wa Argentina kwa misimu minne.

No comments:

Post a Comment