Search This Blog

Wednesday, July 11, 2012

MJADALA: LIONEL MESSI NA RONALDINHO GAUCHO MKALI NANI? - VALDES WA BARCA KAMCHAGUA DINHO.

Kipa wa Barcelona Victor Valdes amesema amecheza na wachezaji wote wawili Ronaldinho na Lionel Messi lakini kwa asilimia 100 anaamini Gaucho alikuwa mchezaji mwenye kipaji kikubwa kuliko wote ambao amewahi kuwashuhudia akiwemo Messi. Kipa huyo mwenye miaka 30, aliiambia Terra TV. Akiwa anatajwa sana kama mmoja ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea ulimwenguni, Messi ameuwasha moto kwenye La Liga katika kipindi cha miaka 8, akivunja rekodi mbalimbali ikiwemo ya kufunga mabao mengi. Lakini, Valdes anaamini Ronaldinho kipekee zaidi aliibadilisha historia ya Barca alipowasili Nou Camp 2003, na kuchangia kwa mafanikio wanayoyapata kikosi cha sasa. "Siku zote nimekuwa nikisema kwamba Rony aliibadilisha historia ya klabu alipokuwa akicheza hapa. Alikuwa kiongozi wa timu ambayo ilibadilisha histori yetu. "Hatukuwa tumeshinda taji lolote kwa miaka mingi. Alikuja na kuifanya Barca kuwa na nguvu na kuifanya kuwa klabu kubwa inayojulikana duniani kote kwa uwezo wake. Namshukuru sana kwa hilo. Naweza kusema ndio mchezaji mwenye kipaji kikubwa kuliko wote ambaye nimewahi kushea nae chumba cha kubadilishia nguo. Alikuwa anafanya vitu vyake vya kustajaabisha kila siku. 

WAADAU MNA MAONI GANI? NANI MKALI

17 comments:

  1. Mimi kwa upande wangu RONALDINHO
    ni mkali tena sana na zaidi ya sana kumzidi huyo anayejiita messi

    ReplyDelete
  2. Messi ni mchezaji bora sana kama ilivyo kwa CR9. Ronaldinho ni mchezaji wa kipekee... alikuwa zaidi ya mchezaji bora... alikaa mioyoni mwetu na alitupa burudani ya kipekee katika soka.. huwezi kuipata tena kwa miaka ya karibuni

    ReplyDelete
  3. SALUM YANGA CHELSEAJuly 11, 2012 at 10:32 AM

    Yaan Ronaldinho ni moto wa kuotea mbali, yaan huyu messi halioni hata vumbi la dinho coz huyu jamaa alikuwa ana vi2 vingi vya ziada, alikuwa ana uwezo wa kuchezea mpira vyovyote anavyoweza yeye me kwa mtazamo wangu dinho ndo mchezaji wangu mkubwa ambaye cjawah kuona zaidi m2 mwenye kipaji hiki amewapita Ronaldo De Lima, Zidane, Messi, Figo na wengineo coz huyu m2 alikuwa hatari sn.

    ReplyDelete
  4. Messi nn nouma jamani afu ukizingatia mgonjwa lakini mambo yake uwiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  5. Gaucho zaidi....

    ReplyDelete
  6. DINO NI HATARI SANA NA NI MTAMU MMNO MESSI ANAWEZA ILA DINO NIFUNDI MKUBWA . KUMBUKA GOLI ALILOWAFUNGA CHELSEA CPL 2004
    PIA MESSI ANA KIKOSI KIZURI KULINGANISHA NA DINNO
    PIA KUMBUKA VITU VYA HUYU MPUUZI WORLD CUP 2002

    ReplyDelete
  7. ronaldinho ni mchezaji ambaye pia alikuwa kipenzi cha wengi wanaopenda soccer ulimwenguni! ila kwa sasa mimi naona muda wake ushaisha na amemuachia bwana mdogo messi! hata ukiangalia pia huko mbele atakuja mchezaji mzuri pia wadau tutasema messi muda wake na ulikuwa uleee!

    ReplyDelete
  8. Messi ni mchezaji bora kwa sasa hilo liko wazi kabisa ila ukimlinganisha na Dinho kwa kweli Dinho alikuwa mkali.Mambo yote anayoyafanya Messi kwa sasa Dinho aliyafanya na zaidi lakini pamoja na hayo mautundu Dinho alikuwa na Mwili na nguvu kitu ambacho messi ana lack.Mimi hata unishikie Bunduki Dinho anabaki kuwa mchezaji Bora kabisa kuwahi kutokea katika soka.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete
  9. Dinho ni balaa kaka. Haijawahi kutokea, alikuwa na uwezo wa KUNYMBULIKA, aliweza kuuchezea mpira alivyotaka, yaani miguu yake ilikuwa kama mikono, aaaah, sijawahi ona kwa kweli.

    Embu mcheki hapa: http://www.youtube.com/watch?v=_dCjy2ye3Xk

    ReplyDelete
  10. Sasa naona mmeamua kufananisha mlango na pazia...gauchooooooooooooooooooooooooo.bhaaaaaaaaaaaaass!!

    ReplyDelete
  11. Messi ni mchezaj mzuri na mwenye manufaa kwa timu yake, anajua kuzitumia nafac vzr na ana uwezo uco wa kawaida ktk ufungaji.
    Ila, ila 2kija ktk raha ya mpira hapo inabidi asubiri kwa Ronaldinho, kwa kweli huyu m2 kadumu ktk kichango cha juu kbs kwa miaka michache ana vi2 vingi ambavyo ni vyake mwenyewe na ameondoka navyo, mnaikumbuka ile chenga yake ya elastic!
    Much Respect kwa Ronaldinho

    ReplyDelete
  12. On my side Messi is the best though kwa ronaldinho kwenye upande wa burudani he
    was the best...but Messi is doing what a striker should be doing and that is score goals...

    ReplyDelete
  13. Mkali ni Dinho mkali ukiangalia soka la one possession of ball ndio utajua kuwa jamaa bado mkali noma yaani

    ReplyDelete
  14. Dinho yupo juu katika ball possession individualy yaan ni kufanisha nguvu ya pawatila na valment katka kilimo

    ReplyDelete
  15. Ronadinho ni mkali sana zaidi ya Messi,alikuwa na vitu adimu mno ambavyo bado hajavifikia

    ReplyDelete
  16. uwiiii huyo messi hawezi kumfikia dino yule ni noma labda kidogo angepambanishwa na CR lakini messi atangoja sana

    ReplyDelete
  17. Dinho ni balaaaaaa.........

    ReplyDelete