Katika kuonyesha kiasi ana demands kubwa kwa mashabiki wa soka. Klabu ya soka ya Hamburg imelalamikiwa na mashabiki kwa kitendo cha kucheza mechi na Barcelona bila kuwepo kwa Lionel Messi.
Huku kukiwa na taarifa juu ya kukosekana kwa wachezaji wengi wa timu ya taifa ya Spain waliopewa mapumziko marefu kutokana na kushiriki kwenye Euro 2012, Messi ndilo lilikuwa jina midomoni mwa mashabiki wengi walionunua tiketi kwa ajili ya mchezo huo. Lakini kwa bahati mbaya Muargentina huyo alipata majeruhi usiku wa kuamkia siku ya mechi na akalazimika kukaa nje ya dimba.
Huku mechi ikiwa imeuza tayari tiketi 57,000, kutokuwepo uwanjani kwa Messi kukawa kama baraka kwa upande wa Hamburg. Pamoja na kuepuka kunyanyaswa na Messi lakini kulikuwa na kifungu kidogo kwenye mkataba kwamba Wajerumani hao wangeilipa Barca €800,000 kwa ajili ya kucheza na Hamburg ikiwa Messi hatocheza, lakini wangetoa €1.2m kama angecheza.
Kwa mujibu wa El Confidencial wameripoti kwamba Messi aliumia baada ya kufanyiwa tackling na mchezaji wa Barca B Marc Barta. Inaripotiwa kwamba Messi alikasirika sana kwa rafu ile na akawa anamfokea kinda huyo.
Muda kidogo baadae katika kujaribu kurudishia rafu, alifanya tackling kwa Barta, na matokeo yake akjiumiza mwenyewe na hatimaye akaigharimu Barcelona €400,000.
No comments:
Post a Comment