Wakiwa wamekasirishwa na kuuzwa kwa Thiago Silva na Zlatan Ibrahimovic kwenda PSG, kundi la mashabiki wa AC Milan walielezea hisia zao za kusikitikishwa na kitendo hicho kwa niaba ya mashabiki wenzao walifanya kituko kikubwa mbele ya ofisi kuu za klabu hiyo.
Kundi hilo la mashabiki lilifanya kitendo cha kuashiria mazishi kwa kuweka kadi ya mazishi, mishumaa na maua mbele ya jengo la ofisi za AC Milan, wakimaanisha klabu hiyo inakufa baada ya kuwauza wachezaji wake bora wawili. Pia baada ya kufanya kitendo hicho mashabiki hao walifungua kesi dhidi ya klabu hiyo kwa madai ya kutangaziwa vitu vya uongo.
Wakati huo huo, klabu imeamua kutoa ofa ya kuwarudishia fedha zao mashabiki walionunua tiketi za msimu waliokasirishwa na kuuzwa kwa Ibra na Silva.
"Uamuzi wa kuwarudishia fedha zao wanunuzi wa tiketi za msimu, hauna uhusiano wowote na kesi tuliyofunguliwa," alisisitiza mkurugenzi Leandro Cantamessa.
"Hii tumefanya kwa wale ambao hawakuwa na furaha, hatuna ulazima wa kuwachezesha au kuwa na wachezaji ambao wanunuzi wa tiketi za msimu wanawataka."
No comments:
Post a Comment