Search This Blog

Tuesday, July 24, 2012

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 1 - 3 AZAM FC - FULL TIME

DK 90: Mpira unaisha hapa uwanja wa taifa, Simba anapigwa 3-1 na Azam FC.

DK 83: Simba 1 - 3 Azam FC

DK 81: Simba wanafanya mabadiliko wanatoka Mussa Mudde na Jona Mkude na wanaingia Salim Kinje na Amri Kiemba

DK 73: John Bocco Adebayor anaifungia Azam bao la tatu - hat trick kwa upande wake.

DK 70: Khamis Mcha Khamis Viali anatoka anaingia Jabir Aziz.

  DK 66: Anatoka Uhuru Suleiman anaingia Kiggy Kakasi.

DK 65: Simba 1 - 2 Azam

DK 60: Kipre Tchetche anatoka anaingia George Odhiambo Blackberry.

DK 53: Shomari Kapombe anaifungia Simba bao la kwanza, moja ya magoli mazuri kabisa kwenye mashindano haya.

DK 46: Mabeki wa Simba wanacheza offside trick na John Bocco anakuwa mjanja na kuuepuka mtego huo anabaki na kipa Juma Kaseja na kumtungua. Simba  0 - 2 Azam.


Second Half: Kipindi cha pili kinaanza hapa uwanja wa Taifa  SIMBA 0 - 1 Azam

DK 45: Azam wanatoka kwenye dakika 45 za kwanza wakiwa wamecheza mpira mzuri sana na wamefanikiwa kuitumia vizuri nafasi waliyopata kwa kufunga bao la kuongoza. Simba inabidi wabadilike hasa kwenye safu ya kiungo na ushambuliaji ambazo leo zimecheza vibaya kwenye kipindi hiki cha kwanza ili kuweza kupata matokeo chanya.

DK 35: Azam wanafanya shambulizi la hatari kwenye lango la Simba na Juma Kaseja anaokoa kichwa safu kilichopigwa na Kipre  Tchetche.

 DK 34: Azam wanacheza vizuri sana kwa dakika hizi, na wanaidhibiti kabisa Simba kwenye nafasi ya kiungo.

DK 30: Simba bado wapo nyuma kwa bao moja, timu zote zinashambuliana kwa zamu huku mpira ukiwa unachezwa zaidi katikati ya uwanja.

DK 25: Simba  0 - 1 Azam

DK 16: John Bocco Adebayor anaipatia Azam goli la kuongoza kwa kichwa, ilikuwa krosi safi iliyopigwa na Shikanda.

DK 12: Simba wanaonekana kuliandama lango la wapinzani wao, Uhuru Suleimani anagongeana vizuri na Mudde anabaki na kipa na anatoa mpira nje.

DK 11: Umahiri wa golikipa Dida Munishi unaiokoa Azam kufungwa bao hapa, lilikuwa shambulizi lilofanywa na Uhuru Suleiman.


DK 07: Felix Sunzu anakuwa mchezaji wa kwanza kupewa kadi ya njano kwenye mchezo huu baada ya kumchezea ndivyo sivyo Balou wa Azam.

DK 05: Simba 0 - Azam 

Kick Off: Mechi inaanza uwanja wa taifa Dsm - Simba 0 - 0 Azam


KIKOSI CHA AZAM KINACHOANZA
1. Deogratius Munishi (27)
2. Ibrahim Shikanda (21)
3. Erasto Nyoni (6)
4. Said Moradi (15)
5. Agrey Moris (13)
6. Kipre Bolou Michael (29)
7. Kipre Tchetche (10)
8. Salum Abubakar (8)
9. John Bocco (19)
10. Ibrahim Mwaipopo (4)
11. Khamis Mcha Khamis Viali (22)

KIKOSI CHA MNYAMA KINACHOANZA
1: Juma Kaseja

2: Shomari Kapombe

3: Haruna Shamte 

4: Juma Nyoso

5: Lino Masombo

6: Mussa Mudde

7: Jonas Mkude

8: Mwinyi Kazimoto

9: Felix Sunzu

10: Haruna Moshi 

11: Uhuru Suleiman

6 comments:

  1. The nice header brings the nice goal well done 'Boko' msula igoma Mwanza

    ReplyDelete
  2. Mtoto yake nepi tuuu!! Good lucky SIMBA

    ReplyDelete
  3. WE MUST KILL THE ANIMAL,,,ndo formular ambayo azamu wanaitumia wanacheza vizuri beki wa simba wanacheza unplaned game Boko anaongeza game:

    Lakini ni makosa ya beki wa Azam tena ndo yanafanyika KAPOMBE SHOMALI anasawazisha goal moja:

    Azam wanatakiwa wacheze kama walivyoanza wamekwisha panic tayali let us see

    ReplyDelete
  4. Poleni sn watani ndo mapinduzi ya soka Tz ila nimesikitika kutolewa mapema nlitaka tukutane fainali ili nikufundishe mpira kwani nisingeshidwa kukufunga goli 7..ila tutakutana tena msimu ujao.

    ReplyDelete
  5. Simba leo wamekufa kabisa, yule sure boy anautaka mpira na kuusambaza anavyopenda. Mtoto atatusaidia Timu ya Taifa.

    Well done Azam, Well done sure boy

    ReplyDelete
  6. AHAAAAAAAAAAAAAAAAAAH VIPI WATANI JAMANI HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHA

    ReplyDelete