Search This Blog

Monday, July 23, 2012

LIVE MATCH CENTRE: YANGA 1 - 1 MAFUNZO - YANGA INASHINDA KWA PENATI 5-3


Mashbaiki wa Yanga wakiongozwa na mchekeshaji Masanja Mkandamizaji pamoja na muimbaji Charlz Baba wakiwa jukwaani kuisapoti klabu yao.

Athumani Iddi Chuji anaifungia Yanga penati ya ushindi na kuipeleka nusu fainali.

PENATI
YANGA - 1, 1, 1, 1, 1
MAFUNZO -1, 0, 1,1,



Mechi sasa itaamuliwa kwa mikwaju ya Penati.

Zinaongezwa dakika 5 za nyongeza.

DK 90: Yanga 1 - 1 Mafunzo

DK  80: Timu zote zinacheza kwa kushambuliana kwa zamu, na zote zinapoteza nafasi za kufunga. Bado 1-1.

DK 72: Yew Berko anaumia na anatoka nje nafasi yake inachukuliwa na Ally Mustapha Barthez.

65: Anatoka Sephano Mwasika anaingia Idrisa Rashid kwa upande wa Yanga. Matokeo bado anga 1 -1 Mafunzo

  DK 55: Yanga 1 -1 Mafunzo

DK 46: Said Bahanuzi anaifungia bao la kusawazisha Yanga. 

 SECOND HALF:  Kipindi cha pili kinaanza Mafunzo wakiongoza kwa bao moja bila dhidi ya mabingwa watetezi.


DK 45: Mapumziko - Mafunzo wakitoka mbele kwa bao moja kwa bila. Timu zote zimecheza vizuri ingawa Mafunzo wameweza kuzitumia nafasi chache walizopata na kuweza kufunga bao ambao limewapa uongozi kwenye dakika 45 za kwanza za mchezo.

DK 40: Mafunzo wanapoteza nafasi ya kufunga bao hapa.

DK 34:  Mafunzo wanapata goli la kwanza kupitia kona - Mafunzo walipata kona tatu mfululizo na wakaweza kuitumia ya mwisho kupitia mchezaji wao Ally Othman Mbanga.

DK 26: Mafunzo wanacheza vizuri kwenye nafasi ya ulinzi lakini wakifika kwenye 18 ya Yanga wanapoteza mipira. Yanga kama kawaida wanaonekana kutulia kila muda unavyozidi kwenda. Matokeo bado ni sare tasa.


DK 23: Yanga wanafunga goli lakini kibendera cha refa wa pembeni kilikuwa juu kuashiria ni offside.

DK 15: Yanga 0 - 0 Mafunzo

DK 10: Yanga wanaonekana kutafuta bao la mapema lakini mafunzo ambao wameingia kwenye mchezo huu wakionekana wanakuja kufungwa - wanaonekana kucheza kwa kutulia bila presha yoyote. Yanga 0 - 0 Mafunzo

DK 5: Yanga 0 - 0 Mafunzo

Kick off: Mechi inaanza hapa Yanga 0 - 0 Mafunzo

Wakati huo huo mechi ya kwanza ya robo fainali imemalizika kwa APR kuwafunga URA 2-1.
Kikosi cha Dar Young Africans kinachoanza leo.

1.Yaw Berko - 19,
2.Juma Abdul - 14,
3.Oscar Joshua - 4,
4.Nadir Haroub Cannavaro (C) - 23
5.Kelvin Yondani - 5
6.Athuman Idd Chuji - 24
7.Rashid Gumbo - 16
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11
10.Hamis Kiiza - 20
11.Stephano Mwasika - 3

Subs;
1.Ally Mustapaha 'Barthez' - 1
2.Godfrey Taita - 17
3.Ladislaus Mbogo - 29
4.Juma Seif Kijiko - 13
5.Idrisa Rashid - 12
6.Shamte Ally - 15
7.Jeryson Tegete - 10

Head Coach: Tom Saintfiet
Assistant Coach: Fred Felix Minziro,
Goalkeeper Coach: Mfaume Athumani
Team Physician: Dr Sufian Juma
Massagist: Jacob Onyango
Kit Manager: Mahmoud Omary (Mpogolo)

12 comments:

  1. Ahsante Brother kwa kutupa matokeo na ninaitakia YANGA ushindi mwema.

    ReplyDelete
  2. Goooo,,,,nice three different corner the third one makes perfect,,

    ReplyDelete
  3. Nice goal they must keep it up

    ReplyDelete
  4. Dah leo kazi ipo kwani Yanga washa wazarau Mafunzo sasa hali isha kuwa ngumu.

    ReplyDelete
  5. Ahsante Mungu kwa Yanga kuweza kusawazisha goli.

    ReplyDelete
  6. Mbona umeweka list ya timu moja tuu?

    ReplyDelete
  7. Ahsante sana Mwenyezi Mungu kwa kuweza kukiskia kiliochetu. Pia napenda kutoa shukrani kwako Brother Shaffih kwa kuweza kutupatia matokeo ya mchezo uliokuwa ukiendelea LIVE. Big up kwa Yanga SC.

    ReplyDelete
  8. Acha uongo Shaffih Yanga wameshinda penati (5-3) aggregate 6-4

    ReplyDelete
  9. APR OYEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  10. TUNAWATAMANI SIMBAAA

    ReplyDelete