Balotelli akiwa na mmiliki wa Bar ya Ocean - Wayne Lineker. |
Mario Balotelli jana usku alivunja rekodi ya matumizi ya fedha kwenye bar wakati aki-party na marafiki pamoja na watoto wa kike huko Ibiza.
Mchezaji huyo wa Manchester City na timu ya taifa ya Italia alikuwa akifanya starehe zake na kundi la marafiki zake katika bar iitwayo Ocean Beach Club, ambayo inamilikiwa na kaka wa mchezaji wa zamani wa England Gary Lineker aitwaye Wayne Lineker.

Mario Balotelli akiwa na warembo kwenye Bar ya Ocean. |
Bar hiyo ni maarufu sana kwa wachezaji wa vilabu vikubwa vya soka, mastaa kama Joe Hart, Andy Carroll, Micheal Carrick na Danny Welbeck, lakini kichaa Balo amewafunika wote hawa kwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa ambacho kinakadiriwa kufikia maelfu ya paundi za kiingereza.
Mmmiliki wa Bar hiyo, Wayne Lineker ambaye pia anamiliki bar kadhaa barani Europa, alitweet kupitia page yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter: Usiku wa balaa in @LinekersIbiza na Mario Balotelli. Bili yake ilikuwa kubwa kuliko zote kwenye bar zangu barani ulaya katika kipindi cha miaka 25 iliyopita."
Balotelli alinunua meza ambayo ya bei ya chini kabisa inakuwa ina gharama ya €5,000, pia aliagiza vitanda maalum kwekwa kwenye eno lake atakalokaa na marafiki zake zaidi ya 20.
No comments:
Post a Comment