Kikosi cha APR kilichoifunga Waw Salaam 7-0 |
Wakati mashindandano ya Kagame Cup yakiwa yanaanza kushika kasi leo nimeanza utaratibu wa kufanya mahojiano na makocha pamoja na key players wa timu shiriki hasa zinazotoka nje ya Tanzania ili kuweza kujua ni namna gani wamejiandaa kupambana kufanya vizuri kwenye mashindano na wanayaonaje mashindano mpaka yalipofikia na mambo mengine mbalimbali kuhusu Kagame Cup 2012.
Kwa kuanzia nilipata nafasi ya kufanya mazungumzo mafupi na kocha wa APR - Ernest Brandy pamoja na mshambuliaji Olivier Kerekezi ambaye alikuwa mfungaji bora mashindano ya msimu uliopita.
Swali: Umejiandaaje kwa mashindano?
Jibu: Tumejiandaa vizuri na malengo ni kufanya vizuri hadi kuchukua Ubingwa. Mashindano haya kwetu ni changamoto kama unavyojua rais wetu (Paul Kagame) ndiye Kombe lake, haitakuwa furaha kama hatutachukua Ubingwa.
Swali: Timu gani unazozihofia?
Jibu: Timu zote ni nzuri na zimejiandaa lakini hofu yangu ni kwa Simba na Yanga licha ya kuanza vibaya, ninachofikiri hatua ya robo fainali na kuendelea zitaleta upinzani kwa timu nyingine.
Swali: Fomesheni gani unapenda kutumia?
Jibu; Napenda kutumia 4-4-2, lakini pia 4-3-3 kulingana na timu tutakayocheza nayo nikiwa na matumaini ya kufanya vizuri na kurudi na kombe nyumbani kwa Paul Kagame.
Olivier Karekezi
Swali: Kama nahodha malengo yenu katika mashindano haya?
Jibu: Malengo ni kufanya vizuri na ninaamini kwa maandalizi mazuri tuliyofanya tutafanikiwa kubeba kombe la 2012.
Swali: Ulikuwa mfungaji bora wa Challenji msimu uliopita, unadhani Kagame 2012 unaweza kufanya hivyo?
Jibu: Inawezekana lakini kila kitu kinakwenda na mipango ya timu katika uchezaji, napenda iwe hivyo ila kubwa ni timu kwanza.
Swali: Timu gani unahisi inaweza kuwapa ugumu kwenye kampenu yenu ya kuchukua ubingwa?
Jibu: Kila timu imejiandaa vizuri naamini lakini tunazidiana, kwa sababu mashindano yanfanyika hapa kwanza lazima niseme kwamba Simba na Yanga nawapa nafasi na nyingine zitafuatiwa - lakini sisi kama APR tumejipanga kupambana mpaka mwisho na tunaamini tuna uwezo wa kuzifunga Simba na Yanga na kubeba kombe kwenye ardhi yao.
aaaah! Lazima waseme hvyo bt kiukwel simba na yanga kiwango bado xana....
ReplyDeleteAngalia mech ya simba na djibout...unadhan watafika wap? 2ache unazi 2elezee hali halisi....
Simba wanasajil ilimrad pasipo kuangalia wanamsajili mchezaj ili acheze wap
2jipange tim ze2 na 2ache siasa kwenye soka na ingekua kila kund zinapita timu mbili 2 siamba na yanga ingekua hati hati....
Ni hayo 2 kwa lolote nichek
0762066086