Chris Coleman amesema itabidi aongee na nahodha wake Aaron Ramsey kabla ya kufikia maamuzi ya kumuita kikosini beki wa Stoke City Ryan Shawcross kwa ajili ya kuichezea Wales.
Kiungo a Arsenal Ramsey alivunjika mguu wake sehemu sita mwaka 2010 baada ya kupigwa tackle ya ajabu na Shawcross, na Ramsey hakupokea kitendo cha mlinzi huyo kumuomba radhi.
Kiungo a Arsenal Ramsey alivunjika mguu wake sehemu sita mwaka 2010 baada ya kupigwa tackle ya ajabu na Shawcross, na Ramsey hakupokea kitendo cha mlinzi huyo kumuomba radhi.
Shawcross mwenye miaka 24 huko nyuma aliwahi kukaririwa akisema kwamba yeye angependa kuitumikia England tu, baada ya kufuatwa na manager wa zamani wa Wales Gary Speed.
Lakini baada ya kutoswa kwenye kikosi cha Roy Hodgson kwenye Euro 2012, manager wa sasa Coleman anajitaarisha kumfuata Shawcross ili aweze kuichezea timu yake, ingawa amesema ataongea na Ramsey kwanza.
"Ryan ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kutupa uimara sana. Nitaongea na Aaron kwa sababu ni mtu ambaye ninamuheshimu, ni nahodha wetu na mchezaji muhimu. Siwezi kuacha kufanya hivi kwa sababu kuna hali isiyoeleweka baina ya wachezaji wawili.
No comments:
Post a Comment