KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima ameondoa hofu mashabiki wa timu hiyo katika kutetea Ubingwa wao wanaoushikilia wa Kombe la Kagame walilolichukua 2011.
Yanga jana walianza vibaya kutetea ubingwa huo baada ya kufungwa na wapinzani wao Atletico mabao 2-0, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Niyonzima alisema, bado wananafasi kubwa ya kulibakisha kombe hilo la Kagame kutokana na uimara wa kikosi chake, mashabiki wanachotakiwa ni kuendelea kuwasapoti ili mechi zinafuata washinde.
Kiungo huyo raia wa Rwanda alisema, anaamini Kocha wao Mkuu, Tom Saintfiet ameyaona mapungufu atakayoyafanyia kabla ya mechi inayofuata dhidi ya Wau Salaam itakayochezwa Jumanne ijayo saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Taifa.
Mrwanda huyo, kipigo walichokipata dhidi ya Atletico ni cha bahati mbaya, badala yake watajipanga kwa kushinda kila mechi watakayokutana nayo ili wafanikishe malengo yao.
mwisho
No comments:
Post a Comment