Search This Blog

Thursday, June 21, 2012

"TUSI LA MCHEZAJI WA 12 KWA UBORA DUNIANI" -NI CHANGAMOTO YA RONALDO KUFANYA VIZURI ZAIDI KWENYE EURO

Cristiano Ronaldo ana kitu cha ziada cha kujituma kuelekea kwenye mchezo wa robo fainali wa Euro 2012 dhidi ya Czech Republic baada ya kuambiwa kwamba hawezi hata kucheza ndani ya kikosi cha kwanza cha timu yake pinzani kwenye La Liga Barcelona.

Kufuatia msimu mzuri na klabu yake, Mchezaji huyo wa Real Madrid  ana matumaini  ya kushinda kombe lake la kwanza la kimataifa na anaamini anapaswa kushinda tuzo ya Ballon d'Or - tuzo ya mchezaji bora wa dunia ambayo kwa sasa inashikiliwa na mchezaji wa Barca Lionel Messi.

Ingawa, Raisi wa Barca Sandro Rosell amesisitiza wiki hii kwamba Ronaldo na kipaji chake kimekuwa kikikuzwa na media lakini sio kweli kwamba ana uwezo ambao unaweza ukamzidi mchezaji yoyote anayeanza kwenye kikosi cha Barca.

"Cristiano Ronaldo sio mchezaji bora wa dunia, anashika nafasi ya 12 . Wachezaji 11 wa kikosi cha Barca ndio wanamuongoza. Nje ya Spain kila mtu anajua na ipo wazi kwamba Lionel Messi  anapaswa kushinda Ballon d'Or lakini sio hapa Spain."

Ronaldo amefunga mabao mengi sana tangu akiunge na Real Madrid kutoka Manchester United miaka 3 iliyopita, lakini mara zote amekuwa akiona jitihada zake zikifunikwa na Lionel Messi, mchezaji wa Kiargentina ambaye yupo njiani kuwa mmoja ya wachezaji bora wa muda wote wa soka.

Kufananishwa kwake na Messi mara nyingi kumekuwa kukimkera Ronaldo, na hiyo ilionekana wiki iliyopita baada ya Ureno kucheza mechi ya pili ya kundi la kifo dhidi ya Denmark, alipokaririwa akisema kwamba hata Messi alifeli mwaka uliopita baada ya kutolewa kwenye Copa America ndani ya ardhi ya Argentina mwaka uliopita.

Perfromance aliyoionyesha Ronaldo kwa kufunga mabao mawili muhimu dhidi ya Uholanzi na kuipeleka timu yake kwenye robo fainali , ambayo ilikuwa kwenye hatari ya kutolewa baada ya kufungwa na Ujerumani kwenye mechi ya ufunguzi.

Kwa mafanikio yake yote kwenye level ya klabu, Ronaldo amekuwa muda mwingine akihangaika kucheza vizuri wakati akiongoza timu yake ya taifa. Alishindwa kuizuia Ureno kufungwa na Ujerumani kwenye Euro 2008 hatua ya robo fainali na haukucheza vizuri wakati Wareno walipotolewa na Spain kwenye robo fainali ya kombe la dunia 2010.

Mechi dhidi ya Czech, timu ambayo imeundwa vizurilakini isiyokuwa na mchezaji mmoja anayetegemewa kama ilivyokuwa miaka iliyopita, timu hii inatoa nafasi kubwa ya Ronaldo na wenzake kwenda hatua inayofuatia ili kuzidi kuongeza nafasi ya Ronaldo kwenye kugombea Ballon d'Or.

Jukumu la kumkaba Ronaldo litatua kwenye mabega ya Theodor Gebre Selaisse, beki mwenye asili ya Ethiopia ambaye alitolewa maneno ya kibaguzi na Russia kwenye mchezo wa kwanza wa Euro  kwenye kundi lao.

Gebre Selaisse ni mchezaji ambaye yupo fiti, ana nguvu na amesema kwamba amejiandaa vizuri kukabiliana na Ronaldo. "Michezo yote kwenye michuano hii imekuwa migumu sana na changamoto kubwa. Ronaldo ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani, lakini hatumuogopi."

Hatua ya robo fainali inaanza leo baada ya siku 12 za hatua ya makundi. Uholanzi ambao walicheza fainali ya World Cup 2010, na Russia waliocheza nusu fainali Euro 2008, ndio pekee walioshangaza kwa kutolewa mapema, na kuifanya hatua ya robo fainali itazamwe zaidi kwa jicho la mbali bila kuzidharau timu kama Greece .

Kuiongoza Ureno sio kazi rahisi kwa Ronaldo, lakini lolote linawezekana ikiwa ataendelea kucheza kama alivyocheza dhidi ya Wadachi. Na kwa kesi hiyo, mmoja ya mabosi wa Barcelona itabidi ale maneno yake mwenyewe.

No comments:

Post a Comment