MAISHA NI NINI
Umaarufu wake katika soka ulianzia katika timu ya Argentina Juniors na taratibu baada ya hapo alizichezea timu za Boca Junior,FC BarcelonaNapoli,Sevilla na Newll's Boys .Amewahi kutwaa tuzo mbalimbali katika maisha yake ya soka na mwaka 2000 alipewa tuzo ya mwanasoka bora wa Karne sambamba na Pele wa Brazili heshima waliyopewa na Fifa.Msomaji wa number10 unajua namna Diego Maradona alivyoishi maisha yakr ya utotoni? Vipi kuhusu uwezo wa familia yake? msikilize Diego mwenyewe katika maala hii ya maswali na majibu.
Swali: Ilikuwaje wakati unajifunza soka?
Maradona; Unajua nilijifunza soka nyuma ya nyumba yetu,kuikuwa na uwanja naotumiwa na timu moja ya daraja la nne,niicheza pale kila siku wakati watoto wengine walipokwenda makwao mimi niliendelea kucheza kwa saa mbili zaid giza likiwa tayari limeshaingia.Nilikuwa sioni kitu gizani ,nilikuwa napiga tu mpira nilichokuwa nazingatia ni miti miwili (magoli).Miaka 10 baadae niliposaini mkataba wangu wa kwanza na Argentina Juniors ndipo nilipobaini uamuzi ule wa kucheza gizani ulikuwa sahihi.
Swali: Wewe ulizaliwa Favel Fiorito,eneo linalosifika kwa umasikini katika jiji la Buenos Aires nini hasa ulichokuwa ukifikiria wakati huo,kwa sababu hujasahau watu wa kule na bado unaendelea kuwa nao karibu?
Maradona; Watu masikini hawawezi kamwe kukuahau au kukulaghai,wengi wao ni marafiki zangu na mmoja wao ni kocha wangu,Coppola,huyu alikuwa akiniibia fedha zangu,watu wa Fiorito wapo katika hali ya umasikini.Leo hii kunaweza kuwa na mambo yanayotoa picha ya maendeleo lakini umasikini bado ni ule ule tangu wakati nikiishi pale,lakini wanasiasa na watu walio karibu na serikali wameendelea kuwa matajiri zaidi na zaidi.Niliwahi kuwa na nafasi ya kuwa kama wao lakini nilikataa kwa sababu ningewaibia masikini,kuna wakati nilizungumza na watu wa Argentina waliojiingiza katika maisha ya sisa na niliwaambia kila kitu ambacho hawakutaka kukisikia.
Swali: Katika maisha hayo ya umasikini,unazungumziaje namna baba yako alivyokuwa akiangaikia familia?
Maradona;Nakumbuka hali ilivyokuwa mara ya baba kurudi kutoka kazini,hakuweza kuwa na chakula cha kutulisha watoto wote sisi nane.Watu walioshiba hawawezi kulijua hilo kamwe,hususani wale ambao hawakuwahi kuwa na njaa,dada yangu alilazimika kula chakula pungufu ili tu chakula kibaki kwa ajili yangu wakati wa jioni kwa mazingira kama hayo unalazimika kuwa na huruma na mwenye kujali wasio na chakula.Historia yangu ya utotoni kamwe siwezi kuisahau hivi hivi,Mama yangu alilazimika kudanganya anaumwa tumbo ili tu aweze kupata chakula kwa ajili ya watoto wake na wakati wote alikuwa akiangalia kwenye mabakuli kuhakikisha kama kuna chakula kwa watu wote.Huo ndiyo umasikini,mama yako analazimika kudanganya,mtu unaweza kuuita uongo wa kisayansi,lakini hiyo ndiyo hali halisi ya maisha ilivyokuwa,nakwambia ukweli.
Swali: Huo ni umasikini kama unavyosema lakini kuna watu wanasahau mapema hali hiyo,wewe vipi unaendelea kuwa na fikra za maisha ya utotoni?
Maradona; Nisingeweza kusahau,sisahau umasikini ni wazamani kuliko utajiri,baba yangu alikuwa akifanya kazi Kvantaca ( eneo la sokoni) na wakati wote alikuwa akibeba mifuko mizito hata wakati ambao umri wake ulikuwa mkubwa.Baada ya kurudi nyumbani Mama alikuwa akimuwekea bonge la barafu shingoni ili kupunguza maumivu na sisi watoto wake wakati huo tulikuwa pembeni,huo ulikuwa kama utamaduni ambao hauwezi kuondoka katika fikra zangu
Swali: Tuzungumzie mambo yaliyozoeleka kwa watu masikini nini hasa unachokumbuka zaidi ukiwa mtoto?
Maradona; Heshima,lakini pia hatukuwa na vitu kama sherehe za kuzaliwa,hatukuwa na fedha kwa mambo hayo,marafiki familia na binamu walikuwa wakikubusu na hiyo ilikuwa zawadi kubwa tu.Hali ni tofauti kwa wale ambao ni matajiri,sina shaka kwamba kuna watu wanaofanya makubaliano na wanasiasa na wanasiasa wanatumia pale wanapohitaji kufanya mambo hayo.Kama wewe hukubali katika utaratibu huo unaonekana kichaa,ndiyo mimi kichaa ni bora niwe kichaa kuliko kukubali nitoe kitu ambacho walitakiwa kunihudumia mimi.Unajua mimi ni kama mtu aliyekufa kwa dakika nne na sasa najua maisha ni nini.
Swali: Kuna walijituma kupunguza umasikini mfano ni mwanamuziki,Bono amezunguka dunia nzima kuwashawishi marais wa nchi tajiri kupunguza madeni kwa nchi masikini na ameweza hata kula chakula cha mchana na aliyekuwa Rais wa Marekani,George W Bush
Maradona; Najua jambo moja ambalo sitoweza kulifanya kamwe ni kupata ujasiri wa kula chakula na Bush,sitaona nimefanya jambo jema kwa kula chakula na muuaji wa halaiki.
Swali: Nini hasa unadhani kifanyike kuleta mabadiliko?
Maradona; Nini cha kufanya?Ni vigumu kubadili mambo,lakini muhimu tuyazungumze matatizo kwanza,bahati mbaya Papa (baba mtakatifu) hataki kuzungumzia matatizo na hata anapofanya hivyo anachofikiria ni kitu kimoja,namna ya kuitunza Vatican kama ilivyo kwa Wamarekani.Vatican ni tajiri sana,dola yao ina ngvu.Papa John Paul II hakuwahi kulifahamu kwa undani kuhusu Afrka,hakwenda pale kubusu ardhi na kuwapa chakula watoto masikini na pia hakuwahi kuijua Argentina.Lakin i ni yeye anayechukua dola million 150 inayotokana na matangazo ya kondomu,asasi inatoa fedha hizo kwa ajili ya kampeni ya matangazo ya biahara,lakini yeye Papa hakuwahi kujua lolote kuhusu kondomu,alikuwa anachukua tu fedha.Leo hii hakuna anayezungumza namna Papa alivyoitupa Afrika na watu masikini wameongezeka tangu kuangushwa kwa ukuta wa Berlin.
Swali: Wewe ni rafiki mkubwa wa rais wab Cuba Fidel Castro,mmekutana vipi na mtu huyu?
Maradona; Mwaka 1987 nilipewa tuzo mbili moja na Cuba nyingine na Marekani,niliwaambia Wamarekani wakae na tuzo yao na moja kwa moja nikaenda Cuba.Nilikutana na Fidel na tukazungumza kwa saa tano kuhusu Che Guevara (mwanamapinduzi wa zamani wa Argentina) .Nikweli nilisoma siku nyingi habar za mapinduzi,busara za Che na Fidel na nikajikuta navutiwa na Fidel na kwa mtazamo wangu yeye ni sawa na Simba anayepigania eneo lake,ni mwanasiasa pekee ambaye hana mtazamo wa kuwaibia masikini.
Swali: Umewaji kusema vita kubwa uliyowahi kupamana nayo ni kuachana na matumizi ya madawa?
Maradona; Ndiyo,ni vita kubwa,lakini ilibidi nipambane nayo kwa bidii na niliamini kuwa ilikuwa vita ngumu,ni kama uko katika mechi ambayo umeshindwa na unataka kushinda kwa namna yoyote ile lakini hakuna msaada wa kupata ushindi nje ya kutimiza majukumu yako.
Swali: Wakati ukichezea Napoli mwaka 1991 ulifungiwa kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu,lakini baadaye ulisema kwamba kufungiwa kwako ni kulipiza kisasi baada ya Argentina kuitoa Italia katika kombe la Dunia mwaka 1990.
Maradona; Naamini hivyo,naamini wale Mafia walikuwa na fedha nyingi sana na walikuwa na hasira na mimi.
Swali: Ilikuwaje hadi ukafungiwa kucheza soka?
Maradona; Walikuta Cocaine kidogo na kunifungia kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja kucheza soka.Hiyo yote naamini ilikuwa sababu ya kunitoa nje ya soka kwa maisha yangu ya soka,walidhani wagenimaliza na kuniacha nimekufa mtaani.
Swali: Uliwaambia nini wachezaji wenzako kabla ya mechi yako ya mwisho ukiwa kama mchezaji mwaka 1997,nasikia wengi walilia!!
Maradona; Ndiyo,wote tulilia nilizungumza na mchezaji mmoja mmoja niliwaaga katika soka na nilifahamu kwamba sitovaa tena jezi nikiwa mchezaji.
No comments:
Post a Comment