Ufaransa ndio ilikuwa nchi ya mwisho kwenda kwenye michuano mikubwa ya kimataifa kama mabingwa wa dunia na ulaya, lakini jitihada za kuwa taifa la kwanza kushinda 'treble' makombe matatu mfululizo katika historia ya soka la kimataifa zilishindikana kwa aibu , baada ya kumaliza kwenye nafasi ya mwisho kwenye kundi A katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2002.
Spain wanajaribu kutengeneza historia kwenye kipindi hiki cha kiangazi. Ingawa maandalizi yao yamekuwa yakiwekwa kwenye wakati mgumu kutokana na majeruhi ya Carles Puyol na David Villa, huku kukiwa na mashaka juu ya form ya Fernando Torres na hali ya kuwa fiti kwa kiungo Xavi Hernandez, kuonekana kutokuwepo kwa hatari yoyote ya kuwatokea kwa aibu ya kutolewa kwenye hatua ya makundi na kurudia historia ya aibu ya wafaransa iliyotokea miaka 10 iliyopita.
Spain kwa sasa wapo katikati ya kizazi chao cha dhahabu: wameshatengeneza na kui-master style yao ya uchezaji, kukava kila sehemu ya dimba, huku wakiwa na mazao ya vipaji vipya (Jordi Alba na wenzie) na vya zamani Xavi na kundi lake, Spain ndio ya kuogopwa zaidi kwenye michuano ya Euro.
Nahodha na golikipa Iker Casillas alisema timu yao inakumbuka sana kipigo walichopewa na Switzerland kwenye mchezo wao wa ufunguzi kwenye WOZA 2012, na sasa wamejipanga kupata suluhisho la namna ya kucheza na kupata matokeo dhidi ya timu ambazo zinapenda kupaki basi golini. Huku Italy na Ireland wakiwa ndio wapinzani wao kwenye mechi zao mbili za mwanzo katika kundi C, Spain watahitaji kupata mbinu mbadala ya kucheza dhidi ya wapaki mabasi.
WACHEZAJI MUHIMU
XAVI HERNANDEZ
Huu umekuwa msimu mzuri kwa Xavi Hernandez binafsi katika klabu yake ya Barcelona, alifunga jumla ya idadi ya magoli 14, ikiwa ndio mara ya pili kufunga idadi ya magoli zaidi ya 9 kwenye misimu 14, lakini huu ndio msimu ambao ameandamwa sana na majeruhi. Tangu alipofanikiwa kuiongoza timu yake kushinda World Cup, Xavi amekuwa akisumbuliwa sana majeraha ya misuli, na japokuwa amehaidi kuwa fiti kwa ajili ya michuano hii, kucheza michezo sita kwenye wiki tatu inaweza ikawa changamoto kubwa kwake.
CESC FABREGAS
Kiungo wa Barcelona amekuwa akianzia benchi kwenye michuano mikubwa miwili iliyopita, lakini mara zote amekuwa akijitahidi na kupata nafasi ya kucheza. Akiwa na miaka 21 kwenye Euro 2008, ilikuwa ni penati yake ambayo iliwaondoa Italia kwenye robo fainali, na alipombadili Villa kwenye nusu fainali dhidi Russia alitoa msaada mkubwa na kuipa ushindi timu yake wa 3-0. Ilikuwa ni stori ile ile kwenye Woza 2010.
Alikuwa ni superb kila alipoingizwa dimbani, na haikuwa suala la kushangaza pale shuti lake ambalo alilipiga na ku-rebound kisha kumrudia Andres Iniesta aliyefunga goli la ushindi kwenye fainali ya kombe la dunia. "Cesc ni muhimu kwenye timu, na anastahili kuwa ndani ya kikosi, lakini kwa bahati mbaya ni watu 11 tu wanaotakiwa dimbani," anasema kocha wa Spain VIcente Del Bosque. "Hata kama anaanzia benchi, hilo halimsumbui Fabregas."
SERGIO RAMOS
Ramos alianza kucheza soka akiwa beki wa upande wa kulia lakini akahama, msimu huu, kwenda nafasi ya beki wa kati. Amefanya vizuri sana kiasi kwamba kocha wake Jose Mourinho ametaka aendelee kucheza nafasi hiyo msimu ujao. "Anapatia sana kucheza nafasi ya kati kuliko beki wa kulia,"anasema kocha wake wa zamani pale Sevilla, Joacquin Caparros. Akiwa na miaka 26, Ramos tayari ameshacheza mechi 83 na Spain, na kutokana na kutokuwepo kwa Carles Puyol, anaweza kujitengenezea nafasi kama mrithi sahihi wa Puyol na kiongozi mpya wa timu.
MASWALIJe Gerald Pique ataweza kucheza vizuri bila Puyol?
Kutokuwepo kwa kombinesheni ya wawili hawa ndio ulikuwa udhaifu mkubwa wa Barcelona msimu huu, inawezekana na ulikuwa ndio udhaifu mkubwa zaidi katika miaka minne ya Pep Guardiola akiwa kama kocha. Barca walifungwa kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya champions league na Chelsea, wakiwa nyumbani wakafungwa na Reala Madrid kwenye mechi ambayo ilimaliza mbio zao za ubingwa wa La Liga. Aliyekuwa amekaa kwenye benchi katika mechi zote mbili alikuwa Pique, ambaye aliipoteza nafasi yake kwenye kikosi kwa Mascherano. Guardiola alihisi Pique ameshika kiwango na kupoteza focus. Sasa kwa upande wa timu ya taifa beki huyu wa kiasili ya kihispania ambaye kwa sasa ana jina la utani la 'Piquenbauer" anahitaji kuirudisha form yake ili kuepusha balaa kwenye safu ya ulinzi.
Je tutaona sana kizazi kipya cha soka cha Spain?
Jibu fupi tu kwa hili ni ndio: wachezaji sita katika kile kikosi cha under-21 kilichoshinda Euro mwaka uliopita walitajwa katika kikosi cha Euro cha Del Bosque, process ya mabadiliko ni nyepesi kwa sababu timu zote za taifa za Spain zinacheza aina moja ya mchezo. Hofu pekee kwa baadhi ya wachezaji ni uchovu: Athletic Bilbao wamecheza mechi 63 msimu huu, mmoja zaidi ya Barcelona, na wachezaji wa Athletic kama Javi Martinez na Iker Muniain wanataka kucheza kwenye Olympics pia kwenye Euro 2012, kama wote wawili watapata nafasi, wakati huo pia bekiwa Valencia Jordi Alba anategemewa kula shavu la kushoto na kuonyesha kwanini Man United na Barcelona zinahitaji huduma yake.

spain watatea kombe lao anaebisha na abishe
ReplyDeletemfumo wa spain unaanza kupotea kama misri hapa Afrika,wasipo jiangalia watakua wakwanza kuaga mashindano..kila la kheli England.
ReplyDelete