Kikosi kamili cha timu ya waTanzania DMV wakiwa na mdhamini mpya wa timu hiyo Mbunifu wa mitindo ya Kwetu Missy Temeke, akiwana na shabiki Didi Vava, katika uwanja wa Greencastle, uliopo Burtonsville, Maryland
Tanzania DMV leo hii iliweza kutinga tena uwanjani kucheza mchezo wake wapili na timu ya Ethiopia, hadi mpira kumalizika timu hizo zimetoka 0-0 katika mpango mzima wa ligi ya 2011 Diaspora World Cup zinazoendelea katika viwanja vya Hyattsville na Germantown jijini Maryland Nchini Marekani.
Mchezaji wa timu ya Ethiopian akipambana vikali na Yousouf Godson Liuzinho, kipindi cha kwanza katika ligi ya 2011 Diaspora World Cupkwenye kiwanja cha Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland.
Wachezaji wa wa timu ya Ethiopia wakiwania Freekick katika dakika ya 62 ya mchezo huo
Benchi ya Timu ya waTanzania DMV wakiwa wanangalia jinsi ya mchezo huo ulivyokwenda dhiti ya timu ya waEthiopia.
Mchezaji wa timu ya Ehiopian akijaribu kumpita beki wa timu ya Tanzania, Emanuel Oumogbao katika mchezo wa pili wa ligi ya 2011 Diaspora World Cup kwenye kiwanja cha Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland.
Jukwa la mashabiki wa timu ya Watanzania DMV, wanne kutoka kushoto akiwa Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV pia alihudhuria katika mpambano huo.
Didi Vava, kushoto akiwa na Sharif Qullatein, Dogo Hudhaifa Shatry, na Mmiliki wa blog ya swahilivilla Abou Shatry, wakiwa katika jukwa la wapenzi wa timi ya waTanzania DMV.
Mdhamini mpya wa timu ya waTanzania DMV ambae ni mwana mitindo na mbunifu wa mitindo ya (Kwetu Fashion Design) Missy Tetemeke akiwa kwenye mpango mzima wa kuangalia na kuiunga mkono Timu ya Watanzania DMV, (Picha ya Kulia) Dogo Hudhaifa Shatry akisikiliza kelele za mashabiki wa timu hiyo.
Mdhamini wa timu ya waTanzania DMV ambae ni mwana mitindo na mbunifu wa mitindo ya Kwetu Fashion Design, Missy Tetemeke akiwa na Bendera ya Taifa.
Benchi la timu ya waEthiopia wakiwa kama mtu nane njee na ndicho kilicho wasaidia kutoka bila kufungana na Timu ya waTanzania DMV.
Didi Vava, katika uwanja wa Greencastle, uliopo Burtonsville, Maryland Sharif Qullatein akiwa na bendera ya Taifa ya Tanzania ndani ya katika uwanja wa Greencastle, uliopo Burtonsville, Maryland
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV pia alihudhuria katika mpambano huo. (Picha ya kulia) Mwana mitindo na mbunifu wa mitindo ya (Kwetu Fashion Design) Missy Tetemeke akiwa na kiongozi wa familia ya Mohammed Matope dogo
No comments:
Post a Comment