Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi atahakikisha mtoto Waleed Kashash anapata matibabu kwa miaka sita ijayo baada ya kutaarifiwa kwamba mtoto huyo wa kimoroko anaugua ugonjwa wa upungufu wa homoni ya ukuaji.
Mtoto mwenye 12 amegundulika kuwa tataizo ambalo limewahi kumkumba Messi huko nyuma atatibiwa kwa fedha ya mshambuliaji huyo baada ya Messi mwenyewe kuamua kufanya hivyo.
Messi akiwa na fulana yenye picha ya Waleed. |
Waleed Kashash, ambaye amegundulika kuwa na ugonjwa huo, ana ndoto za kuja kuwa mchezaji bora wa soka duniani lakini kutokana na kugundulika na janga hilo ndoto yake hiyo ikaanza kufifia.
Ingawa, mwanamke mmoja aitwaye Soad al-Affani aliamua kumjulisha Messi kuhusu ugonjwa huo unaomsumbua mtoto yule, na Messi akamjibu kwa kutoa €208 kila baada ya siku 15 mpaka atakapofikisha miaka 18.
No comments:
Post a Comment