KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Stars Kim Poulsen, amesema kuchelewa kufika kwa wachezaji wake Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wanaokipiga TP Mazembe ya DR Congo, kumetibua programu yake.
Akizungumza jana wakati wa mazoezi ya Stars, baada ya mazoezi ya asubuhi kwenye Uwanja wa Karume, Poulsen alisema kama kikosi chake kingekamilika, lingekuwa jambo zuri.
“Watakapofika Samatta na Ulimwengu, ndipo program zangu zitaanza vema, kwa sasa nashindwa kwa kuwa baadhi ya wachezaji hawajafika,” alisema Poulsen.
Poulsen alisema nyota hao wameruhusiwa na timu yao ya Mazembe leo, hivyo huenda wakatua nchini kesho.
Alisema kutokana na ubora wa wapinzani wao Ivory Coast, anahitaji maandalizi ya kutosha kukabiliana nao, hivyo ni muhimu akawa na kikosi kamili.
Aliongeza kuwa pia kutokuwepo kwa mchezaji wake Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye alienda na msafara kwa ajili ya kwenda kumzika aliyekuwa mchezaji mwenzake Patrick Mutesa Mafisango aliyefariki usiku wa kuamkia Mei 17 kumemchanganya na kusema kuwa akirejea mambo yataenda sawa kwani ataingia kambini moja kwa moja.
Stars inasaka makali ya kuwakabili Ivory Coast katika mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi kwa Kanda ya Afrika itakayopigwa Juni 2, jijini Abidjan.
Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro iko kambini katika Hoteli ya Tansoma toka Mei 15 na itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi ili kujiweka sawa kabla ya kuivaa Ivory Coast ugenini.

No comments:
Post a Comment