Search This Blog

Friday, April 27, 2012

UONGOZI: TUTAWARUHUSU NIYONZIMA NA KIIZA KUONDOKA IKIWA.....

Uongozi wa Yanga umesema upo tayari kuwaachia viungo wake wa kimataifa, Haruna Niyonzima ‘Niyo’ na Hamis Kiiza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu ikiwa klabu zinazowahitaji zitafikia kiwango watakachohitaji.
Kumekuwa na taarifa kuwa viungo hao ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye timu, wapo katika mipango ya kwenda kucheza soka nje ya Afrika, Niyonzima yeye anatarajiwa kutimkia Ulaya wakati Kiiza anaweza kwenda Malaysia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Salum Rupia, alisema wao hawawezi kumzuia mchezaji yeyote kuondoka kwenye klabu hiyo na udai kuwa wanachoangalia ni maslahi mazuri ambayo yatafikiwa.
Rupia amesema licha ya wachezaji hao kuwa na mkataba na Yanga mpaka mwishoni mwa msimu wa 2013/2014, lakini klabu yoyote inayowahitaji wachezaji hao, inatakiwa kufanya mazungumzo na Yanga ili kufikia makubaliano ya dau la usajili.
“Hatuwezi kuwazuia Niyonzima na Kiiza kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, wao soka ndiyo ajira yao, hizo klabu zinazowahitaji ni vema zikafanya mazungumzo na viongozi wa Yanga.
“Bado ni wachezaji halali wa Yanga, mikataba yao inatarajiwa kumalizika msimu ujao wa 2013/2014, hatukatai fedha, tukiwaachia akina Niyonzima na Kiiza tutasajili wengine, wanaowataka bure wasubiri hadi mikataba yao itakapomalizika.”

No comments:

Post a Comment