Pep Guardiola amemaliza uhusiano wake na Barcelona uliodumu kwa miaka takribani 30 baada ya kuwaambia wachezaji wake kwamba msimu ni mwisho kwake kuwepo Nou Camp.
Mhispania huyu, ambaye amekuwa chachu ya kuifanya Barca kuwa moja ya klabu bora kabisa katika ulimwengu wa soka, atamaliza mkataba wake wa kuifundisha timu hiyo ambayo msimu huu imekuwa na wakati mbaya baada ya kulekea kupoteza utawala wa La Liga huku tayari wakiwa wameshavuliwa ubingwa wa mabingwa wa ulaya.
Guardiola kwa sasa atakuwa akiwindwa mno katika soko la makocha duniani - huku Chelsea wakiongoza mbio hizo - lakini imefahamika kwamba mwenyewe anataka kukaa nje ya soka atleast kwa mwaka mmoja.

Mwisho wake ndio umefika |
Kufuatiwa kufungwa na Chelsea jumanne iliyopita na kuelekea kupoteza utawala wa La Liga kwa Real Madrid, kocha huyu mwenye miaka 41 ameitaarifu klabu yake kuhusu maamuzi yake ya kuiacha klabu hiyo.
Mkutano wa waandishi wa habari utafanyika baadae kuelezea kwa undani kuhusu suala hilo.
Guardiola ambaye pia amekuwa akihusishwa na nafasi ya ukocha wa timu ya taifa ya England, alitumia masaa matatu nyumbani kwa raisi wa Barcelona Sandro Rosell jana Alhamisi na aliambiwa kwamba atapaewa kiasi cha pesa kuweza kufanya mabadiliko katika kikosi chake ili kukiongezea uimara kipindi kijacho cha usajili.
Lakini bado, badala ya kukubali kuongeza mkataba pale Nou Camp, Guardiola alimtaarifu Rosell juu ya uamuzi wake wa kutaka kuondoka Barca.
Guardiola kipindi alipokuwa mchezaji wa Barca na kocha wake Bobby Robson |
Guardiola ambaye alizaliwa na kukulia katika eneo la Santepedor, mjini Catalonia, alijiunga na Barca mwaka 1983, ambapo alijiunga na mafunzo mpaka mwaka 1990 alipopata nafasi katika timu ya kwanza.
Alibaki ndani ya timu hadi mwaka 2001na akapata kazi ya kuifundisha kikosi cha Barca B mpaka 2007 kabla ya kuja kuwa kocha wa kikosi cha kwanza mwaka 2008.
Tangu achukue nafasi ya Frank Rijkaard, Guardiola ameiongoza Barca kushinda makombe matatu ya La Liga, mawili ya ulaya, matatu ya spnaish super cup, moja la copa del rey - huku akiwa bado ana fainali ya Copa del rey mwezi ujao, pia ameshinda makombe mawili ya World Club cup na mawili ya UEFA Super Cup - jumla yake yote ni makombe 13.
No comments:
Post a Comment