Ndani ya kipindi cha siku 10 zijazo Barca watacheza mechi 3 muhimu zitazoamua hatma yao msimu huu: watacheza mechi mbili za champions league hatua ya nusu fainali dhidi ya Chelsea pia wana mechi ya jumamosi ijayo ya La Liga dhidi ya Real Madrid.
Mechi zao dhidi ya Chelsea zitaamua hatma yao katika ligi ya mabingwa wa ulaya huku mechiyao dhidi ya mahasimu wao Real Madrid itapigia mstari kuhusu ubingwa wa La liga.
Josep Guardiola siku zote amekuwa akitoa message moja kwa wachezaji wake: "Malengo yetu ni kufika mwezi wa April huku nafasi zetu zote katika mashindano tunayoshiriki zikiwa salama". Kwa mara nyingine tena msimu malengo hayo yamefikiwa, wakiwa tayari wapo katika Spanish Cup, Champions league na La Liga. Siku moja zijazo zitaamua mambo yaweje kwa Barca msimu huu nyumbani na barani ulaya.
Mtihani wa kwanza unaanza keshokutwa dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge. Timu yao imeshawasili London jioni ya leo na watarudi Spain siku ya Alhamisi huku wakiwa wamebakia na masaa yasiyopungua 40 kuweza kuwakaribisha Real Madrid at Nou Camp.
Ikiwa watashinda mechi yao ya El Classico watakuwa wamepunguza pengo la pointi kutoka nne mpaka 1 na kuongeza presha kwa vijana wa Jose Mourinho, kufungwa au kutoa droo kutawapa wakati mgumu sana Barca kuweza kutetea kombe lao. Itakuwa Classico chungu sana kwao.
Siku 3 baadae Chelsea watakuwa wageni katika uwanja wa Nou Camp katika mechi ya pili ya nusu fainali ya champions league. Huu ni mchezo ambao utaamua nani ataenda mjini Munich kucheza fainali.Barca wana changamoto kubwa sana msimu kuweza kuwa timu ya kwanza kuweza kutetea kombe lake la UCL.

No comments:
Post a Comment