Idadi ya wachezaji raia wa Tanzania wanaocheza nje ya nchi inazidi kuongezeka kila siku. Wengine waliondoka bongo wakiwa wadogo na wakaanza kucheza soka nje na wengine waliondoka ukubwani baada ya kukosa nafasi katika ulimwengu wa soka hapa nchini.
Katika ligi kuu ya Kenya kuna mchezaji mmoja anayeichezea klabu ya AFC Leopard Salum Kinje - ambaye kwa sasa anatajwa kwamba ndio kiungo bora kabisa katika ligi kuu ya soka ya KPL.
"Kiukweli huyu jamaa anajua sana mpira namkubali na kumuheshimu sana - nimecheza Tanzania lakini ni bado sijabahatika kuona mchezaji mwenye kiwango cha kumfikia huyu Salum" - Haya ni maneno ya mchezaji wa zamani wa Simba ya Tanzania Jerry Santo akizungumzia kijana Salum Kinje - mtanzania ambaye aliondoka Bongo miaka kadhaa iliyopita kuja Kenya kucheza soka.

Kinje anasema aliondoka Tanzania baada ya kuhangaika sana kuweza kupata mafanikio awakati akiichezea Manyema na baadae Palsons ya Arusha - kabla hajachukuliwa na mkurugenzi wa sasa wa ufundi wa TFF bwana Sunday Kayuni ambaye wakati huo alikuwa kocha wa Coastar Star ya Kenya.
"Nilicheza Costal Star na baadae nikahamia Bandari ambapo nilionekana na timu ya Sofapaka kabla ya kuhamia AFC Leopard ambayo nipo nayo mpaka sasa." - Salum Kinje
Baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika ligi kuu ya Kenya aliitwa katika timu ya taifa ya Harembee Stars lakini baadae walikuja kujua kwamba sio Mkenya hivyo akaondolewa huku akifanyiwa mipango ya kupewa uraia lakini akagoma hivyo mpango wa kuichezea timu ya Harembee ukafa.
"Naamini nina kiwango kizuri na ninaweza kutoa mchango mkubwa kama nikiitwa katika timu ya taifa. Nipo tayari kuitumikia nchi yangu na kuweza kuisadia katika harakati za kupata nafasi ya kufanya vizuri katika mechi za kimataifa."
No comments:
Post a Comment