Search This Blog

Tuesday, April 17, 2012

MWAMUZI MWINGINE WA LIGI KUU YA VODACOM APIGWA HUKO MKOANI DODOMA!






INASEMEKANA HILI BAO LA AGGREY MORRIS NDO LILIPELEKEA MASHABIKI KUMPA KICHAPO MWAMUZI HUYU KWA KILE KILICHODAIWA KUIPENDELEA AZAM KUPATA HILI BAO WAKATI GOLIKIPA WA POLISI ALISHAFANYIWA MADHAMBI!

JAMANI MNYONGE MNYONGENI ILA HAKI YAKE MPATIENI, HILI BAO LILIKUA NA TATIZO GANI ?

2 comments:

  1. Mimi kuna kitu ambacho huwa sikielewi kuhusu hawa polisi wetu ambao huwa wanajaa uwanjani.
    Nina swali moja tu kwao
    1. Huwa wanakwenda kuangalia usalama ama huwa wanakwenda kuangalia mpira?
    Hao mashabiki wote hao wanafanya nini uwanjani na wameingiaje uwanjani wakati wachezaji bado hawajaingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo huko ni kuhatarisha usalama wa wachezaji pia.
    Jeshi la polisi limekuwa likilipwa kwa ajili ya ulinzi ni ulinzi gani ambao wamekuwa wakiufanya kama kazi imewashinda waseme na wawe wanalipa viingilio kama mashabiki wengine, kama vipi TFF wawape kazi mgambo wale huwa hawana ajizi akiambiwa asiingie mtu anafuata oda na ukimletea ujinga unakaa.
    Mimi lawama zangu za kwanza kabisa nazipeleka kwa jeshi la polisi wao walipewa dhamana ya kuhakikisha ulinzi unakuwepo uwanjani ina maana hiyo ni weakness ya jeshi la polisi kwani hawajafanya kazi yao, kwa namna hiyo tunawafundisha nini vijana ambao wana ndoto za kuja kuwa marefaree hapo baadae.
    This is very serious now, TFF amkeni acheni kulaza akilini na kukalia viti tu, kesho na kesho kutwa wadhamini wataanza kujitoa ndio mtatia akili.
    Mdau
    Mike.

    ReplyDelete
  2. Kaka mimi nafikiri ni sahihi kabisa hawa waamuzi kupigwa kwa sababu hufanya mambo ya kipumbavu uwanjani kiasi kwamba watunao kua tumeingia uwanjani tunakereka. Mfano mzuri katika fainali za 9 bora daraja la kwanza kunaupendpleo pale inapocheza polisi Morogoro na timu pinzani hii yote ni kuhakikisha timu inapanda daraja lakini sisi washabiki wa mpira huwa tunataka kushuhudia kiwango harisi cha timu pamoja na wachezaji kwa ujumla. Nafikiri TFF ilifikilie swala la waamuzi kupigwa linatikana na nn na kwa nn waamuzi wapigwe maana hawa waamuzi hufanya walitakaro kutokana rushwa wanazo pewa pasipo wasiwasi kwa sababu TFF haiwafanyi chochote.

    ReplyDelete