Search This Blog

Monday, April 30, 2012

WACHEZAJI WA ZAMANI WA UNITED NA CITY WANASEMAJE KUHUSU MECHI YA LEO: SOMA ALICHOSEMA PAUL INCE

Mchezo wa  168 katika timu mbili kubwa jijini Manchester ndio kwa sasa unaitwa mechi kali na kubwa kuliko zote kati ya timu hizo mbili katika historia ya upinzani wao.

Kuna hatari ya kupoteza kitu na sio tu kombe la Premier league bali pia utawala wa mji katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Wachezaji kadhaa maarufu wa timu hizi mbili wamezungumza juu ya mechi hii.


STEVE BRUCE

Man United  Title winner 1993, ’94, ’96


Nani atashinda derby hii? Siku zote nilijua hii mechi ndio itaamua bingwa. Sidhani kama kungekuwa na utamu kwa hii mechi kama mmoja wao angekuwa juu ya mwenzie kwa pointi nyingi zaidi. City ni hatari sana wakiwa nyumbani lakini United siku zote wanaweza kufanya chochote na popote pale kwa sababu wana uwezo huo.

Matokeo? Nafikiri ni 1-1.

Nani atachukua ubingwa? Pointi moja ya leo itamaanisha United wataendelea kuongoza kwa pointi 3. Sioni ni namna gani wanaweza wakakosea katika mechi zilizobakia. United watachukua ubingwa.

 


 

PETER REID

Man City Player 1989-93 and manager 1990-93


PETER REID
Nani atashinda hii derby? Mtu yoyote ambaye anajiamini kuweza kutabiri matokeo ya mchezo huu yeye ni jasiri sana kama mimi. Timu zote zina wachezaji wazuri - Aguero, Tevez, Silva na Yaya Toure kwa City: Rooney, Welbeck, Giggs and Scholes kwa United. Swali ni wachezaji gani watawazidi ujanja wenzao usiku wa leo.

SCORE: Kama itabidi nifanye utabiri basi nadhani City watashinda 2-1.


Nani Atashinda Kombe: Inawezakana leo City wakashinda mechi na wakashindwa kuchukua ubingwa. Bado wana mchezo mgumu sana dhidi ya Newcastle.


 

PAUL INCE

Man United  Title winner 1993, ’94

PAUL INCE

Nani Atashinda Derby? United watakuwa tofauti leo na mchezo uliopita baina ya timu hizi mbili.City wana wachezaji wengi wanoweza kuamua mechi, United wanae Wayne Rooney. United wameshinda derby nyingi tena kwa uhakika zaidi wakati nipo pale. Ni tofauti sasa.

Score: 2-2

Nani Atashinda taji? Najua United bado wanatakiwa kucheza na Swansea na Sunderland lakini zote kati hizi haziwezi kuwa ngumu kama Newcastle tena wakiwa nyumbani kwa dhidi ya City, na kocha  Alan Pardew ambaye kwangu ni manager wa mwaka. Hivyo hata kama City watashinda leo, United watashinda taji.

 

No comments:

Post a Comment